Chris Brown agombana na meneja wake

0
404

Chris-Brown-550x280MSANII wa muziki wa RnB, Chris Brown, amegombana na meneja wake anayejulikana kwa jina la Mike G, kwa kumtuhumu kuiba fedha zake.

Inadaiwa kwamba msanii huyo alipoteza fedha hivi karibuni huku akiwa na meneja huyo.

Hata hivyo, meneja huyo amesema alikuwa na mpango wa kuachana na msanii huyo hivi karibuni lakini kutokana na jambo hilo atasubiri liishe ili aweze kuendelea na mambo yake.

“Nimefanya kazi na Chris kwa muda mrefu na sijawahi kumfanyia jambo baya, nilikuwa na lengo la kuachana na msanii huyo lakini kutokana na taarifa ya kupotea kwa fedha zake ziwezi kuachana naye hadi nione hatima yake, ila ninaamini sihusiki na jambo hilo.”

Chanzo:Mtanzania

NO COMMENTS