Chadema Warejea Ulingoni Kushiriki Uchaguzi Kinondoni na Siha

0
103

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeridhia na kurejea kushiriki wa uchaguzi mdogo wa wabunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha baada ya kutangaza kuwa hawatashairiki uchaguzi huo mpaka pale mapendekezo yao yatakaposikilizwa.

Uamuzi huo wa kushiriki uchaguzi umetangazwa Januari 19, 2017 na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema kupitia taarifa yake kwa umma.

Kamati Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018. Kusoma zaidi bofya

Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.
Chanzo:GPL

NO COMMENTS