CHADEMA hawatafanya fujo baada ya uchaguzi ikiwa haki itatendeka-Mbowe.

0
931

Mbowe 1Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba, wapiga kura wasikae mita 200 karibu na vituo vya kupiga kura bali waende majumbani baada ya kupiga kura hapo Oktoba 25.

Mbowe aliongeza kueleza kwamba agizo la kuwataka watu hao wapige kura na kurudi nyumbani kulala la sivyo watashughulikiwa na vyombo vya dola si utawala bora.

Akijibu swali kuhusu amani na kuwandaa kisaikojia wanachama kuendelea kuwa watulivu bila kujali nani anashinda, Mbowe alisema, “amani ni muhimu kuliko jambo lolote katika nchi, lakini amani haitapatikani kwa kuvunja sheria na amani hatapatikana kwa woga ila amani itapatikana pale haki itakapotamalaki na utawala wa sheria utakapochukua nafasi yake.”

Kiongozi huyo wa upinzani, aliongeza kwa kusema “Chadema hatukusudii kufanya fujo, hatuna sababu ya kufanya fujo kwasababu tunashinda ila tunataka watanzania wasijengwe na nidhamu ya woga tunavitaka vyombo vyote vya dola na wadau wengine wote wanaohusika na masuala ya haki katika mchakato mzima wa uchaguzi huu wahakikishe kwamba haki ipatikane na ionekane inapatikana.”

Lakini akaonya kama watatumia mamlaka yao vibaya na kuwaonea wananchi , basi hiyo amani inaweza isipatikane .

Aidha alitoa rai kwa Rais Kikwete asihutubie taifa usiku wa mkesha wa kupiga kura kwani suala hilo linaweza kuyumbisha taifa, akitolea mfano kwamba haijawahi kutoka kwa marais wote waliomtangulia nchini humo kufanya hivyo.

Alitolea mfano hotuba aliyotoa wakati wa bunge maalum la katiba, anasema “alivuruga hali ya mambo mpaka taifa likakosa katiba mpya.”

Akizungumzia juu ya ikiwa mgombea wa Ukawa atajiandaa na hotuba mbili ya kushinda na kushindwa, alisema, utafiti unawaonyesha wanashinda kwa zaidi ya asilimia 78, ila hata kama ikitokea wakashindwa ataongea maneno matatu tu na “ hiyo itakuwa ni miujiza” kwa wao kushindwa.

Lowassa anatarajiwa kupiga kura yake huko jimboni kwake Monduli alieleza.
www.voaswahili.com

NO COMMENTS