Archive for the Uncategorized Category
A CELEBRATION OF MUSIC, DANCE & CULTURE FROM EAST AFRICA
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday ShomariDPP sasa akata rufani Lwakatare kufutiwa ugaidi
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Ile kesi ya Lwakatare mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare inaelekea kuchukua hatua mpy baada ya mkurugenzi wa mashitaka DPP kutoa wito mpya kwa mahakama ya rufaa.
Kwa taarifa zaidi ungana na gazeti lw Mwananchi Kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake, Joseph Ludovick Rwezaura, sasa imetua Mahakama ya Rufani, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuiomba mahakama hiyo kuingilia kati.
Lwakatare na Rwezaura, walikuwa wakikabiliwa na kesi ya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka hayo na kubaki na shtaka la kula njama.
Hata hivyo, DPP amewasilisha maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani akiomba iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwafutia mashtaka ya ugaidi. Kusoma zaidi bofya Read more »
RAIS KIKWETE AWAKARIBISHA TIMU YA TAIFA KWA CHAKULA CHA JIONI NA KUWATAKIA BAHATI NJEMA JUU YA MCHEZO WAO NA MOROCCO
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars Nadir Haroub ‘Canavaro’ baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam na kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco utakaochezwa Juni 7 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars, Tasso Mukebezi, akiteta jambo na Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete Alhamisi mchana.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa hisani ya Michuzi
SERENGETI FREIGHT WACHANGIA HARAMBEE WATOTO WENYE KANSA LONDON
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Mheshimiwa Balozi akiwa na muandaaji wa shughuli mama Balozi
Wazee wa kazi wakiwa pamoja na Mheshimiwa Balozi .
Kulikuwa na mnada na bahati nasibu ambapo vitu bali mbali vilinadiwa kutunisha mfuko.
Dada mtanzania alijishindia tiketi ya VIP kwenda kumuona Alicia Keyys pale O2 arena.
Chris Lukosi alijishindia zawadi ya miwani ya Gold.
Flaviata Matata atoa wito kwa serikali kuhusu ajali ya MV Bukoba
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Na Mwandishi Maalum.
MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameiomba serikali kutangaza Mei 21 ya kila mwaka kuwa siku maalum ya maombolezo ya wasiku maalum ya maombolezo ya wahanga wa MV Bukoba.
Ajali ya MV Bukoba ilitokea Mei 21 mwaka 1996 na kuua watu zaidi ya 1,000 na serikali kutangaza siku tatu za maombolezo ya kutokana na kuzama kwa meli hiyo iliyotokea kwenye Ziwa Victoria. Katika ajali hiyo, Flaviana alipoteza mama na kaka yake.
Flaviana ambaye kwa sasa anafanya shughuli za kuonyesha mitindo nchini Marekani na Uingereza, amekuwa mstari wa mbele kuadhimisha siku hiyo kwa kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation.
Akizungumza Kwa niaba ya Flaviana Matata Mkurugenzi wa Compass Communications Company Limited Maria Sarungi Tsehai alisema pamoja na ajali hiyo kuua watu wengi, lakini inasikitisha kuona jambo hilo kwa sasa limekuwa kama kumbukumbu kwa wahanga wa ajali hiyo tu na si vinginevyo.
Maria ambaye alisema hayo katika misa maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo iliyofanyika kwenye makabuli ya Igoma, Mwanza alisema kuwa wakati umefika sasa wa kutangaza siku ya kitaifa ya maombolezo na kwani ajali hiyo imeacha Watanzania wakiwa na huzuni kubwa.
Alisema kuwa wanashukuru sana kwa miaka hii miwili wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa Marine Service Company Limited na kampuni ya ndege ya Fastjet, ambapo mwaka jana walikabidhi vifaa vya kujiokolea (maboya) 500.
WABONGO JUU-JAY Z KUPIGA SHOW DAR OCTOBA 4
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Jay Z ametoa mlolongo wa shows zake atakazopiga kwa wiki 7 kuizunguka dunia kwa dhumuni la kuleta ufahamu juu ya tatizo la maji. Tour hii ndefu itaanza Septemba 9 huko Krakow, Poland. Jay Z atadondoka Dar na atagonga show hiyo tarehe 4 Octoba pale Diamond Jubilee. Na hii ndio list ndefu ya tour ya Jay Z:-
Sept. 9: Krakow, Poland (Coca-Cola SW Live Festival)
Sept. 10: Bratislava, Slovakia (Incheba)
Sept. 15: Amsterdam (Heineken Music Hall)
Sept. 16: Germany (TBA)
Sept. 18: Istanbul (Refresh the Venue)
Sept. 19: Athens (Olympic Arena)
Sept. 21: Manchester, England (Evening News Arena)
Sept. 22: Glasgow (SECC)
Sept. 23: Birmingham, England (National Indoor Arena)
Sept. 24: London (Wembley Arena)
Sept. 26: Dublin (the Point)
Sept. 27: London (Royal Albert Hall)
Sept. 29: Paris (Le Zenith)
Sept. 30: Milan (Fiera di Milano)
Oct. 2: Barcelona (Teatro Heineken)
Oct. 4: Dar es Salaam, Tanzania (Diamond Jubilee)
Oct. 6: Accra, Ghana (Accra Conference Center)
Oct. 7: Lagos, Nigeria (Ocean View)
Oct. 9: Luanda, Angola (Cine Karl Max)
Oct. 11: Cape Town, South Africa (Belleville Velodrome)
Oct. 13: Durban, South Africa (ABSA Stadium Outer Fields)
Oct. 14: Johannesburg (Coca Cola Dome)
Oct. 17: Hong Kong (TBA)
Oct. 18: Bangkok, Thailand (BEC Tero Hall)
Oct. 20: Seoul, Korea (Walker Hill Gayagum Concert Hall)
Oct. 21: Taipei, Taiwan (Taipei Dome)
Oct. 23: Singapore, Singapore (Suntec City Concert Hall)
Oct. 25: Sydney (Entertainment Centre)
Oct. 27: Brisbane, Australia (Entertainment Centre)
Oct. 28: Melbourne (Rod Laver Arena)
JAY Z AKANUSHA BEYOUNCE SI MJAMZITO
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday ShomariTangazo la Mkutano wa Injili Washington DC
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday ShomariALEX LUKETE ALONGA NA VOA KUHUSU NAFASI ZA MASOMO VIU
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari 
Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA) ilizungumza na mratibu wa wanafunzi wa kimataifa katika chuo cha Virginia International University (VIU) huko Fairfax Virginia Bw.Alex Lukete na katika mazungumzo hayo ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na jinsi gani wanafunzi wa nje wanaweza kupata msaada wa kimasomo (Schorlaship), pia anazungumzia kuhusu ajira wanawasaidia vipi wanafunzi wao kuweza kupata ajira?, halikadhalika hata wale walio nje ya nchi wanaweza kusoma chuoni hapo bila kusafiri kwenda Marekani. Je ni kwa staili gani msikilize kwa kubofya hapa.
MSIBA DMV NA TANZANIA
Posted in Uncategorized on May 23, 2013 by sunday Shomari
Martin Ngireu Enzi ya Uhai Wake
Familia ya Ngireu inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa baba yao Martin Ngireu kilichotokea siku ya Jumanne Mei 21, 2013 katika Hospitali ya Holy Cross iliyopo Silver Spring, Maryland, nchini Marekani.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Donalson Funeral Home, iliyopo 313 Talbot Avenue, Laurel MD na kutakuwa na Misa na kumuaga marehemu siku ya Jumamosi Mei 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 10 jioni (12- 4 pm) kwenye addres 313 Talbot Avenue, Laurel, MD baada ya hapo kutakuwa na chakula kwenye address 210 Patuxent Road, Laurel MD.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inafanywa na kama ilivyo desturi yetu kupeana pole ndiyo ustaarabu wetu. Msiba upo 210 Patuxent Road, Laurel MD kuwapa pole watoto wa marehemu Carol na dada yake waliokuja kutoka Tanzania. Msiba huu ni wetu sote DMV tafadhali tujumuike na tuwafiriji wafiwa. Kushirikiana na kushikamana kwa shida na raha ndiyo staili na maisha yetu DMV.
Kwa maelezo na maelekezo tafadhali wasiliana na mtoto wa Marehemu Carol 301 957 4523.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe!






