Buriani Elizabeth Edwards

0
428

Mapambano na kansa ni magumu yamedhihirisha kuwa ni magumu sana baada ya wiki hii dunia kumpoteza mwanaharakati na mtetezi wa wanyonge hapa Marekani Bi Elizabeth Edwards kwa ugonjwa wa Kansa.

Ama kwa hakika huu ni ugonjwa ulio peleka watu wengi sana kutoka hapa duniani ukiwa unauwa kwa haraka kuliko hata UKIMWI, wiki hii dunia imempoteza Elizabeth Edwards

Edwards ambaye kama mama yangu alipambana na ugonjwa huu na kuwataka wananchi wajue kwamba hakushindwa mapambano bali amefika mwisho wa maisha yake kwa usalama.

Nikiweka orodha ya waliopoteza maisha yao kwa ugonjwa huu ni kubwa sana tu, ama kwa hakika kazi ipo ya kupambana na ugonjwa huu hatari . Bi Elizabeth Edwards atakumbukwa kwa mengi kama mama mlezi,mwanasheria na mpigania haki za watu wa chini alikuwa mhimili wa mume wake katika mapambano ya kuwania nafasi ya urais.

Watu wengi wanamwona si tu kama mke wa mgombea urais bali yeye ni kama mgombea mwenyewe alikuwa mshauri mkuu wa mume wake na wachamnbuzi wanamwona alikuwa ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa kiasi kwamba angeweza kuwa mgombea yeye mwenyewe na kushinda nafasi yoyote katika serikali.

Anasemekana amekuwa ndio nguvu kubwa ya mafanikio ya kugombea nafasi ya urais na makamu ya wa rais mwaka 2004 na pia ameonyesha kuwa mwanamke mwenye uvumilivu mkubwa baada ya kashfa ya mume wake kuwa na mwanamke wa nje na kuandika kitabu chake Resiliance.

NO COMMENTS