Buriani Dr. Remmy Ongala

0
735


Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi Tanzania Dr. Remmy Ongala amefariki dunia jumapili nyumbani kwake Sinza kwa Remmy mjini Daressalaam Tanzania eneo ambalo limepewa jina lake.

Dr. Remmy Ongala ambaye alizaliwa nchini Congo 1947 alipewa jina hilo kutokana na umaarufu wa nyimbo zake zilizoonekana kuwa ni za utetezi kwa wanyonge na alijiita hivyo sikuzote. Lakini alichukua uraia wa Tanzania baada ya serikali kumpa kashi kashi za kutaka kumfukuza nchini humo hasa baada ya kuonyesha ukosoaji mkubwa kwa serikali na kutoa nyimbo ya kumsifu kiongozi wa upinzani aliyekuwa maarufu sana Augustine Lyatonga Mrema ambaye sasa ni mbunge wa Vunjo.

Dr.Remmy ameugua ugonjwa wa kisukari katika muongo uliopita na pia ulimzuia kushiriki katika tamasha la Muziki la WOMAD ambalo hufanyika London kila mwaka ugonjwa huo ulipelekea kupooza.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alikwenda kumtembelea hospitali hivi karibuni. Wimbo wake Kifo ulipata umaarufu mkubwa na hivi leo unapigwa sana katika radio za Tanzania kumuenzi mtaalam huyu wa muziki.

Dr.Remmy Ongala aliingia Tanzania kwa mara ya kwanza 1977 na kujiunga na Ochestra Super Makassy. Sikiliza kipande cha muziki wake maarufu Kifo. Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi. Amen.

NO COMMENTS