Bryan Mwombeki ashinda mpira wa Tennis Capital Junior OPEN # 1 L 5 Washington, Dc

0
505

IMG_0394Bryan Mwombeki (kati kati) akiwa na kombe lake la ushindi pamoja naye ni nduguze KageBriana na Bryton Mugisha.

Mtoto Bryan Mwombeki ameshinda Kombe la watoto la michuano ya Tennis mjini Washington,DC kwa kuwa mshindi wa kwanza kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi (10) ulioandaliwa na S.Marie Tournaments chini ya Shirikisho la Tennis Marekani (USTA) na kufanyika katika viwanja vya ndani vya Tennis SETLC , SE Washington DC.

Bryan aliwashinda wapinzani wake, Bryce Freeman bao 4-2,4-2 kisha akamshinda Lucca Gandolfo bao 4-0, 4-1 na kupata ushindi wake mkubwa dhidi ya Carel Ngounoue bao 3-5,4-1,10-5.

Mtoto Brian pia ni mpiga kinanda maarufu wa misa ya Kiswahili DMV.

NO COMMENTS