Bernard Hopkins bado wamo

0
375


Bondia mkongwe wa Marekani Bernard Hopkins Jumamosi alishindwa kutimiza ndoto yake ya kuwa bingwa mzee kuliko wote duniani baada ya kutoka sare na bondia wa Canada Jean Pascal.

Hopkins ana miezi michache kufikisha 46 alikuwa avunje rekodi ya George Foreman ambaye alikuwa bingwa katika umri wa miaka 45 baada ya kumtwanga Michael Moore na kuchukua mkanda wa uzani wa juu duniani.

Jaji mmoja alimpa ushindi Hopkins 114-112 lakini majaji wengine wawili walimpa droo na kupelekea pambano hilo kuamuliwa kuwa ni sare. Hopkins ambaye aliangushwa mara mbili katika raundi ya kwanza na ya tatu aliwasha moto wa mashambulizi kuanzia raundi ya sita na kuendelea ambapo Pascal alionekana kuishiwa na gesi.

Hopkins amelalamika kuwa alistahili ushindi na kuuliza si kuanza pambano kuwa ni muhimu bali ni jinsi unavyomaliza na akauliza mpaka mwisho nani alikuwa mchovu kati yao? Pascal na nani alirusha makonde mengi kuliko mwenzake na yakaingia Hopkins! nani alikuwa hoi ? Pascal sasa alitaka wajaze wenyewe nani mshindi.

Lakini mpaka mwisho wa siku pamoja na Hopkins kutokuondoka Quebec Canada na mkanda ameondoka na heshima na ana haki ya kupata pambano la marudiano kwao hapa Marekani. Bernard Hopkins kwa ujumla amelalamika kuwa kanyimwa ushindi hasa baada ya kudai alipigwa nyuma ya kichwa alipoanguka kwa mara ya kwanza na Pascal kupewa pointi hizo. Wakati yeye alimwangusha Pascal katika raundi ya 11 lakini refa akasema Pascal ameteleza tu kwa hiyo Bernard hakupewa pointi hiyo.

Bernard Hopkins (kushoto) akila konde la Jean Pascal

NO COMMENTS