Baraza la Mawaziri lasubiriwa kwa hamu Tanzania bara

0
673

Rais Jakaya kikwete

Rais Jakaya Kikwete yupo kwenye hatua za mwisho kuunda serikali yake, baada ya kumteuwa waziri mkuu Mizengo Pinda kuendelea nae katika awamu ya pili sasa suala ambalo wachambuzi wengi wa siasa za Tanzania wanaelekeza macho yao ni kwenye baraza la mawaziri.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika mwandishi Dina Chahali alisema “uteuzi wa Pinda ulitarajiwa na watanzania wengi kutokana na utendaji wake na rekodi yake nzuri”. Rais Kikwete anatarajiwa kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri na pia kutokana na kuanguka kwa baadhi ya mawaziri kuanguka katika kinyang’anyiro cha kugombea ubunge, kwahiyo wanatarajia mabadiliko makubwa katika baraza hilo.

Katika kipindi cha kampeni za kugombea urais, moja ya sera zilizopigiwa debe na vyama vya upinzani ni kupunguza baraza la mawaziri ili kubana matumizi ya serikali. Kwa hiyo anatarajiwa kuwa atakuwa na baraza dogo la kusaidia kuendesha serikali ili kutimiza kama ahadi yake. Pinda kwa mujibu wa Dina aliwashukuru wabunge akisema kama anavyoitwa “mtoto wa mkulima” lengo lake kubwa ni kuwakomboa masikini nchini humo ambao wengi wanaishi vijijini na wengi wao ni wakulima.

Je Rais Kikwete atateuwa baraza la mawaziri la aina gani? itakumbukwa awamu ya pili ya Rais Ben Mkapa aliahidi kuteuwa baraza la mawaziri la wachapa kazi akiwafananisha na askari wa miavuli lakini kwa mshangao wa watanzania wengi walikuta akiteuwa mawaziri wakongwe na vigogo wa zamani waliokuwa hawategemewi kurudi kwenye baraza hilo ili waongoze wizara zake. Sasa je Kikwete itakuwaje tunasubiri.

NO COMMENTS