Baraza la mawaziri lasubiriwa kwa hamu: Sura mpya ni zipi?

0
491

Rais Jakaya Kikwete
Nchini Tanzania baraza jipya la mawaziri linalotarajiwa kutangazwa wiki hii na Rais Jakaya Kikwete linasubiriwa kwa hamu kubwa baraza hilo kwa mujibu wa gazeti la mwananchi linatarajiwa kuwa dogo na lenye ufanisi mawaziri wachache. Vyanzo vya habari kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi vimeeleza kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.

Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita.

Chanzo cha habari hiyo kimeeleza kuwa Rais Kikwete amekataa kuwapa nafasi ya uwaziri wabunge waliopata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi mkuu uliopita.

Wabunge wanaotajwa kuingia katika baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza ni Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Kilango (Same Mashariki).

Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa rais katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni Mweka Hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa).

NO COMMENTS