Barack Obama arudi upya!

0
361


Baada ya kuonekana mgawanyiko mkubwa kwenye bunge la Marekani na kupoteza ushindi kwa wabunge wa democrat na mabishano makali ya kumpinga Obama bungeni na hatimaye Obama kukubaliana na wabunge wa republikan juu ya unafuu wa kodi kwa matajiri uliotolewa na utawala wa Bush ilionekana kana kwamba Obama amepoteza kabisa umaarufu wake.

Lakini bunge la Marekani jumatano hatimaye lilipitisha mpango mpya wa kupunguza silaha baina ya Marekani na Russia na moja kwa moja kumpa Rais Barack Obama ushindi mkubwa katika sera yake ya mambo ya nje.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) bunge hilo lilipiga kura kwa kura 71 kwa 26 kuunga mkono mpango mpya wa START jumatano. Mpango huo utapunguza idadi ya silaha za nyuklia zinazomilikiwa na Marekani na Russia na kuweka mpango wa pamoja wa kuthibitisha silaha hizo.

Aliwashukuru maseneta wademocrat na warepublikan kwa kupitisha kile alichokiita kuwa ni suala lake la juu la usalama wa taifa. Hivyo Obama ameonyesha kurudi upya baada ya kushindwa kwa chama chake vibaya katika uchaguzi wa kati kati ya muhula aliouita “Shalacking”.

Lakini kwa namna fulani sasa ameonyesha uwezo wa kufanya makubaliano na wabunge wa republikan na hatimaye kumpa ushindi wa kupitisha masuala makuu muhimu katika ahadi zake za uchaguzi kupunguza silaha za hatari za nyuklia, pia wamepitisha muswaada wa kuwaruhusu mashoga kutobaguliwa katika jeshi la Marekani na kutoa fedha za kuwezesha matibabu ya bure kwa waathirika wa taka za sumu zilizotokana na mashambulizi ya Septemba 11,2001.

Na cha kufurahisha kwa wamarekani wengi ni kwamba haya yote yamefanyika katika kipindi cha muda mfupi tu.

NO COMMENTS