BALOZI ADADI :AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANS

0
203

BALOZI
ADADI :AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA
SAYANSI

Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi
Adadi
Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza
imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule
zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia
ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu
Sekondari wilaya hiyo  Julitha Akko

Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya
Sekondari
Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la
Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara
walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za
sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa
nchini

MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani
Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za
Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya
sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa
nchini.


Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara 
kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya
ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa
chini.


Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao
ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika
shule ya sekondari ya Muheza.


“Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali
la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa
zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma
kwa bidii “Alisema.


Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika
vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka
wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na
sera ya viwanda.


“ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo
niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika
matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma
kwa bidii “Alisema


Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara
katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza
kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu
ili kuona namna ya kulimaliza.


Awali akizungumza katika hafla hiyo, Afisa elimu sekondari wilaya Muheza
Julitha Akko amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopatiwa
vifaa hivyo kuacha tabia ya kufungia ndani ya makabati na badala yake
vitumike kama ilivyokusudiwa.


Aidha alisema kuwa lazima kuwekwe utaratibu wa namna ya kuvitunza vifaa
hivyo na kuagiza visitumike kinyume na makusudio yake na kuwataka
wanafunzi waelekeze nguvu zao kwenye masomo ili kuongeza wataalamu
wengi.


Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Muheza(Muheza high school)
Alex Birumo alisema yapo mategemeo makubwa ya kuongeza ufaulu hasa kwa
masomo ya sayansi kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo
wanafunzi walikosa fursa kwa miaka mingi kujifunza kwa vitendo.


“Shule yetu hii ni ya masomo ya sayansi ya michepuo ya PCB NA CBG na ni
ya kidato cha tano na sita unapokuwa na wanafunzi zaidi ya 150
unawafundisha bila ya vifaa vya maabara kiukweli mafunzo yetu kwa
wanafunzi hao yahakuwa na tija”Alisema
Habari kwa hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha

NO COMMENTS