BACK TO LIFE SOBAR HOUSE: JAMII ISIWATENGE WAHANGA WA DAWA ZA KULEVYA

0
541
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Jamii
nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake
wawasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo
vya utimamu wa akili (Sobar House).
Rai hiyo ilitolewa wiki hii na Eddy Darkis ambae ni Meneja
wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House kilichopo Pasiansi Manispaa
ya Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho kinawasaidia wahanga wa dawa za kulevya
kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Darkis alibainisha kuwa badhi ya wanajamii
wamekuwa wakiwanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya, jambo ambalo
linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Kwa mwaka 2015, zaidi wahanga 50 wa dawa za
kulevya waliokuwa katika Kituo hicho kutoka Mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa
ikiwemo Mkoani Mwanza, wamerejea katika hali zao za kawaida baada ya kupatiwa
tiba ya kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya huku wengine zaidi ya 25
wakiendelea kupatiwa tiba katika kituo hicho.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu nchini
(OJADACT) Edwin Soko, Idadi ya Watumiaji wa dawa za Kulevya Jijini Mwanza
imefikia zaidi ya Watumiaji Elfu Kumi katika kipindi cha miezi sita iliyopita
huku sababu za ongezeko hilo zikiwa ni kutokana na kukosekana kwa njia
mathubuti za kupambana na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana
na wanaojihusisha na biashara ya dawa hizo mara kwa mara kubuni mbinu mpya za
usafirishaji jambo linalosababisha ugumu katika kupambana na biashara hiyo.

NO COMMENTS