BAADA YA FLORA, MISS TANZANIA…SKENDO YA MBASHA, MKE WA MTU YATIKISA

0
221

Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha akiwa na anayedaiwa kuwa mke wa mtu.

DAR ES SALAAM: Baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Flora Mbasha kisha kudaiwa kuanzisha uhusiano na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa na kumwagana, muimbaji wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amejikuta akitikisa kwa skendo ya kuhusishwa na mke wa mtu.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo, kwa muda mrefu Mbasha amezua minong’ono na mwanamke huyo ambaye inasemekana ni rubani wa ndege kutokana na picha na jumbe za mafumbo ambazo Mbasha amekuwa akiziweka mitandaoni. “Mbasha kwa kweli ametikisa kwa muda mrefu. Tumefuatilia sana picha anazoposti mtandaoni hususan akiwa na huyo mdada ambaye inadaiwa ni mke wa mtu, anaonekana kabisa kuna kitu lakini pengine hataki kukiweka wazi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kuna siku alimweka huyo mdada katika Insta (Instagram) yake, akamtakia heri ya kuzaliwa lakini watu walikuwa na maswali mengi kutokana na sifa alizompa mdada huyo japo kuna watu wengine walisema ni rafiki yake wa kawaida tu.”

Risasi Jumamosi liliperuzi katika ukurasa huo wa Instagram na kushuhudia maoni mbalimbali ya wafuasi wa mtandao huo ambao walionesha kumtilia shaka mwanamke huyo wakihoji kama kweli ni mke wa mtu iweje ajianike hadharani na mwanaume mwingine Hata hivyo, wapo wengine ambao waliwataka wale wanaotilia shaka ukaribu wao, waache kuropoka mambo wasiyoyajua kwani ‘kumuwishi’ mtu bethidei ni jambo la kawaida.

Katika mazungumzo mengine na mwanahabari wetu, chanzo chetu kilieleza kuwa, ukiachana na picha ya kumtakia bethidei mwanamke huyo, ilivuja picha nyingine ambayo ndiyo imewafanya watu wazidi kumtilia shaka Mbasha na mwanamke huyo ambaye anatajwa pia kuwa na mkwanja mrefu. “Hiyo picha ndiyo balaa.Kusomza zaidi bofya

Mbasha anaonekana yupo ndani ya gari upande wa dereva huku mke wa mtu akiwa upande wa kushoto lakini safari hii, huyo mke wa mtu kajisogeza hadi kifuani kwa Mbasha wakawa very close kama mtu na mtuwe. “Katika hali ya kawaida, marafiki tu wa kawaida au mtu ambaye mnaheshimiana, hamuwezi kugandana kwa staili ile, itakuwa kuna kitu cha ziada tu kinaendelea,” kilidai chanzo hicho. Baada ya picha hiyo kutua dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alijaribu kumtafuta mke huyo wa mtu bila mafanikio kwani simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipoulizwa Mbasha kuhusu mwanamke huyo na kutumiwa picha yake, alikiri kumfahamu kama rafiki yake lakini akaweka wazi kuwa hana uhusiano wowote mbaya. “Tafadhali sana jamani naomba muwe waungwana, huyo dada tunaheshimiana sana na siwezi kufanya kitu chochote kibaya na ukizingatia mumewe pia tunaheshimiana, ngoja nikutumie picha ya yeye na mumewe.

Nawaheshimu sana jamani hao,” alisema Mbasha na kumtumia mwandishi wetu picha mwanamke huyo akiwa na mumewe. Hata hivyo Mbasha hakuwa tayari kumuelezea kwa undani mwanamke huyo, mwandishi wetu alipotaka kumfahamu zaidi.

NO COMMENTS