
Jumatatu May 20, 2013 VIJIMAMBO italonga na Rais wa Vizion One, Inc, Bw. Abdallah Kitwara. Naye ataelezea maisha yake kwa ufupi, shule alizosoma na alishawishika na nini kufungua kampuni na kwanini alitumia jina VIZION yenye Z badala ya S. Mbali na Vizion One, Inc ana kampuni gani nyingine hapa nchini Marekani na Tanzania.Kaa stan by.
USIKOSE KUMSIKILIZA.
Author Archive
VIJIMAMBO ITALONGA NA ABDALLAH KITWARA
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday ShomariMaadhimisho ya miaka 4 Ibada ya Kiswahili Columbus – Ohio
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday ShomariPROFESA J AFUNGUKA
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday Shomari
Joseph Haule a.k.a Professa J.
Profesa Jay au Joseph Haule ni mmoja wa wasanii maarufu na wanaoheshimika nchini Tanzania katika mazungumzo na funguka na Risasi wiki hii aliulizwa kuhusu sakata kati ya Judith Wambura ‘Jide’ na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Clouds Media, Ruge Mutahaba. Profesa Jay naye ametajwa katika sakata hili Fuatilia mazungumzo yao hapa.
Funguka: Mambo vipi Profesa, nimekutafuta ili nipate msimamo wako kwenye bifu kati ya msanii mwenzako (Jide) na Ruge.
Profesa Jay: Kwanza nianze kusema kuwa mimi sina upande wowote ambao ninaweza kuusimamia, sipo kwa Ruge wala kwa Jide.
Funguka: Kumekuwa na minong’ono mitaani kuwa upo upande wa Jide kwani mmekuwa mkifanya kazi pamoja vilevile ni marafiki kwa muda mrefu na ndiyo maana amekushirikisha kwenye wimbo wake wa Joto Hasira. Unalizungumziaje hili?
Profesa Jay: Ishu siyo mimi kuwa upande wa Jide au wa Ruge, kitu ambacho ninaweza kukizungumzia ni kwamba Jide alinishirikisha kwenye wimbo huo hata kabla ya hilo bifu lao sijalifahamu. Mimi niliimba kutokana na maudhui ya wimbo ulivyokuwa ukitaka. Kwa hiyo bado nasisitiza kuwa sifungamani na upande wowote katika jambo hili.
Funguka: Kama ni hivyo, unachukuliaje suala la Jide na Ruge kufikia hatua ya kuburuzana mahakamani?
Profesa Jay: Kuhusu hilo, sitakuwa msemaji sana ila kwa jinsi ninavyofahamu, Jide ni msanii mkongwe. Kama unakumbuka nilishawahi kufanya naye traki kadhaa kama Bongo Dar-es-salaam na Niamini. Kikubwa ni kwamba Jide anajiheshimu sana na nadhani kila anachokifanya anakijua vizuri.
Funguka: Unamuongeleaje Ruge na uongozi mzima wa Clouds kuhusu sakata hili?
Profesa Jay: Binafsi siwezi kuwaongelea Clouds au Ruge kwa jambo lolote, kwa sababu ninaamini na wao ni watu wazima na wanafahamu nini wanachokifanya.
Funguka: Hivi karibuni tumesikia wasanii kadhaa wamejitoa kwenye orodha ya wasanii watakaomsapoti Jide kwenye shoo yake ya Mei 31, vipi wewe utakamua kama kawaida?
Profesa Jay: Nikutoe wasiwasi, mimi binafsi nitakuwepo kwenye shoo ya Jide na nitapiga mzigo wa kufa mtu kumsapoti kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na moyo wangu wote.
Funguka: Poa, nashukuru kwa ushirikiano wako, kazi njema.
Profesa Jay: Haina kwere.
LEO NDIO LEO KATI YA LAMONT PETERSON NA LUCAS MATTHYSE
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday Shomari
Lucas-matthysse wa Argentina.
Lamont Peterson wa USA.
Lamont Peterson ana mtihani mkubwa Jumamosi atakapopambana na Lucas Matthyse wa Argentina huko Atlantic City NJ. Kwa wengi wanaomfahamu Peterson watakubaliana nami kuwa huyu ni mmoja wa mabondia hatari kwa sasa.
Katika orodha ya mapambano magumu aliyoshinda ni pamoja na bondia hatari wa Uingereza Amir Khan, Victor Manuel Kayo, Kendal Holt, na kutoka sare na Victor Ortiz na amepoteza pambano moja tu.
Ila safari hii anakutana na bondia mwenye rekodi ya kutoa watu knock out au KO , huyu kijana mwenye asili ya Argentina ana nguvu sana na huwa anaogopeka kwa hilo.
Katika mapambano 33 aliyopigana 31 kati yake ameshinda kwa KO na hayo mawili pekee ndio alipoteza.
kwa hiyo leo ndio leo na mpambano huu utaonyeshwa moja kwa moja na Show time.
YANGA YAPELEKA KILIO MSIMBAZI
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday Shomari
Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo. Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano ‘Messi’, Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude
Yanga line up: Ally Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Athuman Idd ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima. Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz na Jerry Tegete
Mpira unaanza uwanja wa Taifa
Dkk 1 YELLOW CARD…! Mbuyu Twite wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Haruna Chanongo wa Simba
Dkk ya 4 Didier Kavambagu anaipatia Yanga bao la kuongoza
Dk 8 Simba inapata kona ambayo haizai matunda
Dkk 10 Didier Kavumbagu wa Yanga anamchezea faulo Shomari Kapombe.
DkK 15 bado Yanga wapo mbele kwa goli 1-0
Dkk 16 YELLOW CARD……! Haruna Shamte wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Simon Msuva.
Dkk 20 Cannavaro wa Yanga anachezewa faulo na Haruna Shamte wa Simba.
Dk 21 Hamis Kiiza wa Yanga anauwahi vizuri mpira katikati ya mabeki wa Simba waliojichanganya kuokoa lakini shuti lake hafifu linaokolewa na kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosaDk 27 PENALLLLTTY……! Simba inapata penalti baada ya Cannavaro kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.
Dk 32 Mwinyi Kazimoto wa Simba anamchezea vibaya Frank Domayo wa Yanga.
Dk 35 Kiiza wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya mpira alioupiga kutoka juu ya lango la Simba.
Dk 38 Simba inapata kona ya pili.
Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 – 0 Simba SC
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza
Dkk 63 Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili
Dkk ya 75, Young Africans 2 – 0 Simba SC
Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
Dkk ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
Dkk ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.
Mpira umemalizika, Young Africans 2 – 0 Simba SC
Kavumbagu ddk 4
Kiiza dkk 63
BLUE IVY KUPATA MDOGO WAKE?
Posted in Uncategorized on May 18, 2013 by sunday Shomari
Mwanamuziki maarufu Beyounce Knowles Carter inaripotiwa kuwa yu mja mzito, hayo yalikuja kutokana na nyota huyo wa “Single Lady” kutangaza anavunja ziara yake ya kimuziki huko Ulaya akidai sababu ni uchovu.
Tour hiyo ya nchi za Ulaya iitwayo Mrs. Carterambayo ilikuwa imalizikie hapa Marekani.
Hivi karibuni alipohojiwa ABC alisema kuwa angependa kuona mwanaye anampata mdogo wake wa kucheza naye.Pia aliongeza kwamba angependa kuwa na familia kubwa.
Habari ndio hiyo na ilithibitishwa na (ET).
Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kuwepo kwa sera na Sheria mpya unapaswa kupingwa-Zitto Kabwe
Posted in Uncategorized on May 17, 2013 by sunday Shomari

Kesho jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia. Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo.
Ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 22 – 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii ni maandalizi ya Bajeti hii.
Jambo la kushangaza ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na ndio kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, Serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya Mafuta na Gesi kwenye Bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.
Zabuni hii mpya ya vitalu vya utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge kuzuia ugawaji huu mpya mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi vikamilike.
Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi?
Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria mpya unapaswa kupingwa Kwa Nguvu zote.
Tafuta mbunge wako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali.
Tumalize kwanza sera na Sheria ndio tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.
Naomba tureje statement yangu ya mwaka jana September 2012:
URL: https://zittokabwe.wordpress.com/2012/09/10/oil-and-gas-in-tanzania-building-for-a-sustainable-future-a-call-for-a-moratorium-on-new-offshore-exploration/
Oil and Gas in Tanzania: Building For A Sustainable Future
A Call for a moratorium on new offshore exploration.
Tanzania is on the precipice of an economic evolution with the recent discoveries of gas.Kusoma zaidi bofya Read more »
FAINALI MISS UTALII TANZANIA 2013, KUFANYIKA JUMAPILI MKWAKWANI TANGA
Posted in Uncategorized on May 17, 2013 by sunday Shomari
Hatimaye fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani Tanga siku ya Jumapili Tarehe 19-5-2013katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Fainali hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii
Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, zitajumuisha jumla ya warembo 30 kutoka mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90, 000,000/=,ambao unajumuisha skolashipu ya kusoma kozi ya Diploma katika chuo cha Dar es Salaam City Collage, safari za kushiriki mashindano ya Dunia,ziara za Tanzania Great Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri wakati wa shughuli za kutekeleza majukumu yake ya ushindi,na shilingi 5,000,000/= baada ya kutumikia taji lake wakati wa kukabidhi kwa mshindi wa msimu ujao.Kusoma zaidi bofya Read more »
KATIBU MUHTASI AFUNGUKA NA KUSEMA VIONGOZI NDIO WANAOTOA SIRI ZA NCHI SI WAO.
Posted in Uncategorized on May 17, 2013 by sunday Shomari
CANDICE GLOVER NDIO MSHINDI WA AMERICAN IDOL 2013
Posted in Uncategorized on May 17, 2013 by sunday Shomari
Candice Glover hatimaye alichukua ushindi wa American Idol 2013 Alhamisi usiku, baada ya kushiriki kwa mara ya tatu katika show hiyo.
Candice Glover amethibitisha msemo wa atafutaye hachoki hata akichoka keshapata.
Alipoulizwa nini cha kusema alijibu miaka mitatu akiwa na maana muda alioendelea kujaribu kabla ya kupata ushindi.
Lakini ushindi huu ulitabiriwa na wengi kwenye mitandao ya kijamii nilipouliza swali hilo Jumatano.Hongera Candice.




