ASKOFU MDEGELLA ATAKA WATANZANIA KUMWOMBEA RAIS MAGUFULI.

0
1812

Askofu 
wa kanisa la Kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa
Dr OwdenBurg  Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto   Monica
Kasesela huku babake mkuu  wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na
binti yake  Cathelin Kasesela  wakishuhudia baada ya kumalizika kwa
ibada ya pili katika  usharika wa kanisa  kuu

Askofu Dr Mdegela  akitoa  baraka

Dereva  maarufu  wa Taxi eneo la Posta  mjini Iringa Bw  Sisico  akiwa katika vazi la Christmas

 Mwalimu  wa kwaya ya  vijana katika kanisa
kuu Bw Lupyana Samweli akipokea  baraka  za Christmas kutoka kwa
askofu  wa kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi 
ya  Iringa Dr OwdenBurg Mdegela leo   mara baada ya  ibada

 Askofu
wa kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi  ya 
Iringa Dr OwdenBurg Mdegela akimpa  baraka za Chritmas mlemavu ambae ni
mwimbaji maarufu wa kwaya  ya vijana  kanisa kuu  Gift Mwanuka

 Vijana  wa kanisa  kuu  wakiwa katika  maombi

 Maombi  maalumu kwa Taifa la Tanzania

 Kwaya   kuu  wakiimba

 Kwaya  kuu  wakiimba  wimbo maalumu

 Mkuu  wa  wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela  kulia akiungana na  waumini wa kanisa la  kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa  kuu  kuliombea Taifa na  serikali ya  Rais Dr John Magufuli

 Waumini wa kanisa la kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT)  usharika wa kanisa  kuu wakiliombea Taifa wakati  wa ibada ya Chritsmas

 Askofu Dr Mdegela akitoa salamu  za Christmas  leo

 Askofu Dr  Mdegella  akitoa  baraka  kwa  waumini  wa kanisa kuu leo

Askofu 
wa kanisa la Kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa
Dr OwdenBurg  Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto   Monica
Kasesela huku babake mkuu  wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na
binti yake  Cathelin Kasesela  wakishuhudia baada ya kumalizika kwa
ibada ya pili katika  usharika wa kanisa  kuu

Na MatukiodaimaBlog

 WAKATI
waumini wa Dini ya kikristo hapa nchini leo wakiungana na wakristo wenzao
kote ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo ,
Askofu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg
Mdegella amesifu amani iliyotawala nchini kutoka uchaguzi mkuu hadi
sasa na  kuwaomba  watanzania  kumwombea Rais Dr John Mapuguli kwa kuleta mabadiliko  ya kweli  ambayo hata  wapinzani  walikuwa wakiyataka.


“Salamu zangu na maelezo yangu ni mafupi  kila mmoja anafahamu Burundi na  Kenya   walifanya uchaguzi  na  hadi  leo hii bado  wanauana  na maisha yanakuwa magumu……ninyi mnafahamu awamu ya kwanza kuja  ya  pili  tumevuka salama ,awamu ya  pili  kuingia  ya tatu  pia salama na awamu ya nne kuingia  ya tano  ndio  tumevuka  salama  salimini  zaidi  kuliko awamu nyingine  zote…..kwa  nilitaka  kuasema hata  wale  waliotumia mabomu  na  kutumia gharama  kubwa wakati wa uchaguzi nafikiri  walikuwa  wamekosa mazoezi kwa  muda mrefu ya kutumia mabomu hayo  bila  sababu  Watanzania ni  wapenda amani”

Askofu Dr Mdegella alitoa kauli hiyo wakati wa ibada hiyo ya christmas iliyofanyika katika kanisa kuu  kuwa hadi  hapa  sasa Bwana Mungu ametusaidia  na  sio  amesaidia uchaguzi  tuo hata mambo mengine ambayo tulikuwa tunayataka kwa kuzungusha  mikono kuwa mabadiliko sasa yamekuja.

Alisema   kuwa  Mungu  si  kaibadilisha Tanzania na  kuipa  neema  katika  uchaguzi mkuu pekee kwani kila  mtanzania  kwa  sasa anaona mabadiliko kawaida  ukilinganisha na awali kwani  wakati  wa kampeni watu  walikuwa  wakizungusha  mikono kama ishara ya kutaka mabadiliko na mabadiliko  yameanza kuonekana kwani  matajiri  walikuwa wamejitajirisha mno na masikini  walikuwa  wamekumbatia  umasikini  wao .

“Kulikuwepo  pengo kubwa kati ya matajiri na masikini kwani matajiri  walijitajirisha  zaidi na masikini  waliendelea  kubaki masikini ila  sasa kwa kipindi  kifupi  cha serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli mabadiliko  ya  kweli  yanaonekana “

Askofu  Dr Mdegella mbali ya  kumpongeza Rais Dr Magufuli kwa utendaji mzuri na baraza lake la mawaziri bado  alitaka uzi huu wa kutumbua majibu ambao unaendelea uzidi kukazwa zaidi ili kila  mtanzania aweze kufaidi  matunda ya nchi  yake .

 ” Sasa  ombi langu kwenye watanzania najua Francis Godwin utaandika naomba kila  mmoja  wetu  bila  kujali  ulimpa kura ama  ulimnyima tuzame  katika maombi kumwombea Rais wetu  ili mabadiliko  yaendelee  na nchi  iwe na amani na maendeleo pamoja na mafanikio …kwa  wale  waombolezaji naomba leo  kuombeleza  kumshukuru  Mungu na  sisi  wote   kuungana kumwombea  Rais  wetu  na tarehe 3 Januari 2016  wote  kutoa  shukurani ya pekee  kumshukuru kwa kuvuka  salama katika uchaguzi na kuendelea  kuona neema hii ya  utendaji wa Rais wetu pia kazi ya  kutumbua majibu iwe  endelevu kwa wakubwa na  wadogo ….ukimkamanda mtu  mwenye msokoto mmoja  wa bangi na  kumwacha  mwenye gunia la bangi ikome  japo  sisemi mwenye msokoto mmoja asikamatwe wote  washughulikiwi ” 

Alisema
kuwa watanzania ni watu wanapenda amani na utulivu na ndio maana
wamepata kupita katika wakati mgumu wa uchaguzi mkuu pasipo kutokea
machafuko yoyote.

” Kati ya
vipindi vigumu ambavyo watanzania tumepitia kwa amani na utulivu ni
pamoja na kulinda amani wakati wa uchaguzi mkuu na kuingia katika
sikukuu hii ya chritmas bila amani kuvurugika”

Hata
hivyo alisema kuwa amani hii watanzania tumeipata bure na kuwa kuzaliwa
kwake Yesu Kristo  kubisha hodi kwa kila mmoja wetu ili aweze kuingia
ndani ya mioyo ya wote hivyo Kazi kubwa kumfungulia ili aweze kuingia
ndani ya mioyo yetu.

Alisema kuwa Yesu Kristo amekuja ili kufanana na wanadamu wote na kuwa njia pekee ni kumpokea pasipo kushindana na Mungu .

Huku mkuu  wa  wilaya  ya  Iringa Bw Richard  Kasesela  ambae  alipata  kushiriki ibada   hiyo alimpongeza askou  huyu Dr Mdegella kwa  kumpongeza Rais Dr Magufuli na serikali ya  awamu ya  tano na  kuwa moyo huo  wa  viongozi  wa  dini unapaswa  kuendelea zaidi kwani kauli  zao zinasikilizwa  zaidi.

Bw Kasesela  alisema amependezwa na askofu huyo  kutenga  muda  wa  kuiombea  serikali na  kudai  kuwa kazi kubwa inayofanywa na   viongozi wa  serikali ya Dr Magufuli akiwemo waziri mkuu na baraza la mawaziri pamoja na watendaji  wengine ni nzuri na kila mtanzania anaiona   hivyo zawadi kubwa kwa watanzania ni sala na dua  zao .

MWISHO

NO COMMENTS