Arethra Franklin agunduliwa na Kansa

0
331

Aretha Franklin

Mwanamuziki mkongwe Arethra Franklin “Queen wa Soul” ametangazwa kutibiwa Kansa ya wengu huko Detroit Michigan. Televisheni moja ya Detroit imeripoti habari hizo. Pi imeripotiwa kuwa alifanyiwa upasuaji Alhamisi na kwamba anaendelea vizuri ambapo alitembelewa siku ya Jumatano na Mchungaji Jesse Jackson.

Alipohojiwa Malkia huyo wa Soul aliyetamba na nyimbo nyingi ikiwamo “You make me feel like a Natural Woman” alisema Mungu anamsimamia katika kila jambo “nimekuwa na madktari wazuri na manesi ambao walibarikiwa na sala zote za mji huu na nchi nzima kwa ujumla”. Hivi sasa malkia huyu wa miziki ya soul amekatisha ziara yake ya kimuziki.

Tunamtakia uponyaji wa haraka na kila la kheri-Arethra Franklin.

NO COMMENTS