Amber Rose ataka mtoto wa pili na Wiz Khalifa

0
387

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Amber Rose, ameweka wazi kuwa anataka mtoto wa pili ili mtoto wake wa kwanza apate mdogo wake.

Mrembo huyo alifanikiwa kupata mtoto na rapa, Wiz Khalifa, mtoto wao kwa sasa ana miaka mitatu anajulikana kwa jina la Sebastian.

Hata hivyo, mrembo huyo anadai kuwa atakuwa na furaha zaidi kama atafanikiwa kuzaa na baba mtoto wake, Wiz Khalifa.

“Nipo tayari kupata mtoto wa pili kwa ajili ya mwanangu awe na mdogo wake wa kike au wa kiume azidi kuwa na furaha, ninaamini ninaweza kufanya hivyo lakini natamani nizae tena na Wiz Khalifa,

“Bado nina uhusiano wa karibu lakini si wa kimapenzi, natarajia kumwambia kama atakuwa tayari anizalishe mtoto wa pili,” alisema Amber Rose.

Chanzo: MtanzaniaAmber-Rose-206x300

NO COMMENTS