ALIYEKUWA KATIBU MWENEZI WA TANU AFUNGUKA MAZITO!

0
319

Dk. Fortunatus Lwanyantika Masha ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa TANU akafukuzwa Agosti 1968 amesema, hakujua kwa nini alitimuliwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na Global Tv, Sengerema, Mwanza, mzee Masha alisema mkutano wa Halmshauri Kuu ya TANU ulioketi Tanga ndio uliofanya uamuzi wa kuwafukuza chama bila kupewa nafasi ya kujitetea yeye na wenzake tisa.
“Kabla ya kufanyika mkutano ule mimi nilijua kuwa tutafukuzwa lakini nilidhani tutaitwa ili kujitetea lakini haikuwa hivyo,” alisema Dk. Masha.

NO COMMENTS