Ali Kiba apeperusha bendera ya Tanzania duniani

0
495

Mwanamuziki wa Tanzania Ali Kiba akishirikiana na wasanii wengine maarufu wa Afrika na mtaalam R.Kelly msanii wa Marekani hatimaye ameshiriki kutengeneza hii video ya kimataifa.

Katika mahojiano yangu yaliopita na wasanii wa Tanzania Klynn, Ali Kiba, A. Y a.k.a “Mzee wa Commercial”, Mwana Fa na Profesa Jay a.k.a Heavy weight Mc nilizungumza nao kuhusu uwezekano wa wasanii wa Tanzania kushirikiana na wanamuziki wa Marekani.

Maana wasanii hawa huenda Tanzania mara kadhaa na kufanya matamasha lakini wasanii wa Tanzania huishia kuwafungulia pazia bila kupata faida yeyote sasa Ali Kiba amefanikiwa kupeperusha bendera ya Tanzania .

Pongezi nyingi kwa Ali Kiba na blog hii itaendelea kumtafuta ili tufanye naye mahojiano kupata habari zaidi za mpango huu wa One 8 na R.Kelly.

NO COMMENTS