Agness Gerald ‘Masogange’ kafikishwa tena Mahakama ya Kisutu

0
85

Video Queen Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye ametokea kwenye video kadhaa za muziki wa Bongofleva, leo July 25, 2017 alifikishwa Mahakamani Kisutu Dar es salaam kwa mara nyingine kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili.
Mahakama ya Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza kesi hiyo kutokana na Wakili wa Serikali kuuguliwa na mtoto ambapo ilielezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili kutolewa ushahidi aliambiwa kuwa Wakili wa Serikali ambaye anatakiwa kusikiliza kesi hiyo anauguliwa na mtoto wake.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi August 2, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY