Waziri wa fedha wa Tanzania azungumza na ubalozi Washington Dc

0
558
Waziri wa fedha na uchumi wa Tanzania Bw.Mustafa Mkulo alipozungumza na wafanyakazi wa ubalozi Washington Dc mwishoni mwa juma

Waziri wa fedha na uchumi wa Tanzania Bw.Mustafa Mkulo amesema kuwa Tanzania imejipatia mikopo isiyopungua kiasi cha shilingi za kitanzania 397.5 bilioni kutoka benki ya dunia.

Alisema hayo katika mkutano wake na Balozi wa Tanzania mjini Washington Dc uliohudhuriwa pia na baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi huo na ujumbe wa Tanzania uliokuja kwenye mikutano ya benki ya Dunia na IMF.

SHARE
Previous article
Next article

NO COMMENTS