Kenya yaimarisha usalama baada ya shambulizi la Garissa.

0
421

KDF
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Joseph Nkaissery amewaambia waandishi wa habari Alhamisi usiku mjini Garissa kwamba operesheni iliyoanza mara tu baada ya shambulizi kutokea mjini humo imemalizika.

Mkuu wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet, ametoa amri ya kutotoka nje wakati wa usiku katika kaunti nne za mashariki, ikiwemo Garissa. Amri hiyo inatarajiwa kudumu kwa takriban wiki mbili ikiwa mojawapo ya hatua za kuimarisha usalama.

Shambulizi la Alhamisi lilikuwa na mauaji makubwa kuliko lile la mwaka wa 2013 kwenye eneo la maduka ya kifahari ya Westgate mall mjini Nairobi, ambapo wanagambo wa Al-Shabaab waliokuwa na silaha waliwaua takriban watu 67 katika muda wa siku kadhaa.

Kundi hilo la wanamgambo linaloaminika kuwa na makao yake nchini Somali, limedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo lilianza muda mfupi kabla ya alfajiri katika chuo kikuu cha Moi , tawi la Garissa.

Maafisa wa usalama wanasema washambuliaji waliokuwa na silaha walivamia lango la chuo hicho na kuua walinzi wawili, kabla ya kuzingira mabweni na kuanza kuwafyatulia risasi wanafunzi huku wakiwashikilia wengine mateka.
VOASWAHILI

NO COMMENTS