Dunia itamkumbuka sana Shujaa Arrow buriani

0
463


Mkongwe wa muziki wa Soca Rhumba aliyetamba katika miaka ya 80 maarufu kama Arrow alifariki dunia tarehe 15 septemba 2010 akiwa na umri mdogo wa miaka 60. Jina lake kamili ni Alphonsus Celestine Edmund Cassell na alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 10 tu.

Mwaka 1967 alianza kuimba peke yake na mtindo wa Soca Callypso na alipewa jina la Jr.Monarch .

1969 Alikuwa mshindi wa pili katika mashindano ya Callypso King Competetition.
1972 Alitoa nyimbo single ya kwanza “Dance with Me Woman”
1974 Alitoa albam ya kwanza “The Mighty Arrow on Target”
1975 Alitoa albam “Arrow strikes again”.
1982 Alitoa Kibao kilichotamba “Hot hot hot”.
1983 Albam “Heat” na single “Rub Up”.
1984 Alitoa Albam “soca savage” ikiwa na wimbo Long time ulitamba katika anga za kimataifa na kukamata Top 30 Uingereza.
1986 “Heavy Energy iliyochanganywa na vionjo vya kilatino Merengue”.
1988 “Knock them Dead” album ya kwanza chini ya Island Records.
1988 Alipata tuzo ya Living Legends kutoka kwa waandaaji Bodi ya Utalii Bahamas na Carribean Song Festival.
2007 Alishiriki kwa mara ya mwisho alishiriki kuimba kwenye mashindano ya dunia ya Cricket pamoja na Byron Lee, Shaggy na Kevin Little.

Atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na ubunifu wake mkubwa kuchanganya Callypso au muziki wa Carribean na R&B na Salsa licha ya ukosoaji kuwa alikuwa anaharibu Callypso lakini watu wengine walimwamini kuwa analeta mabadiliko na alifanikisha kwa upande wao.

Atakumbukwa kwa nyimbo yake 1983 Hot hot hot ambayo ilikamata namba 59 kwenye chati za juu za muziki Uingereza, Groove Master no.23 na 1989 Ola Soca no.38 hapa Marekani ,

Wimbo wake Hot hot hot ulikuwa wimbo wake wa kwanza kuuza kimataifa na pia wimbo uliouza kwa kiasi kikubwa sana wa soca duniani na wimbo uliotumika kwenye kombe la dunia huko Mexico 1986.

NO COMMENTS