Siasa za Zanzibar zachukua mtazamo mpya

0
687
Mgombea wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad
Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha

Uchaguzi Zanzibar safari hii unaelekea kuchukua sura mpya tofauti na miaka mingine kampeni za uchaguzi visiwani zimekuwa tulivu na hakuna mvutano wala mapambanao kati ya wafuasi wa chama cha CUF na CCM ambao ndio mahasimu wakubwa visiwani humo. Hii kwa kiasi kikubwa imetokana na kura ya maoni visiwani humo ya serikali ya umoja wa kitaifa kati ya vyama hivyo vikuu viwili.

Hivi karibuni mgombea uwakilishi wa CCM wa Mwanakwerekwe na Waziri Kiongozi wa Zanzibar Bw.Shamsi Vuai Nahodha amediriki kusema kuwa CUF au Maalim Seif amekiri kushindwa kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 31 aliongea hayo kwa mujibu wa gazeti la Habari Leo katika mkutano wake wa kampeni hivi karibuni akisema kuwa Maalim Seif amekiri kuwa Dr.Shein ni kiongozi mwenye uwezo na yuko tayari kufanya naye kazi.

Itakumbukwa kwamba suala la muafaka Zanzibar limekuwa ni kitendawili kwa muda mrefu baada ya CUF kudai mara kadhaa kuwa wanaibiwa kura zao na CCM na kukataa kumtambua rais wa Zanzibar Bw.Karume lakini hivi karibuni alipokuwa akikaribia kumaliza muhula wake wa uongozi alifanya mazungumzo ya faragha na Maalim Seif na hatimaye yalipelekea Maalim Seif kutangaza ghafla kuutambua uongozi wake suala ambalo lilitaka kuleta mtafaruku kwenye chama cha CUF.

Lakini baada ya kuwaelewesha wanachama wake basi hatimaye walitoa tamko rasmi la kuutambua utawala wa rais Karume na hata kuthubutu kusema aendelee madarakani kwa muhula wa tatu ili waweze kumalizia masuala ya muafaka lakini CCM ilikataa na kuahidi yeyote atakayeshika madaraka atafuata nyayo hizo.

Na hatimaye wananchi wa Zanzibar walipiga kura kutaka kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa na tangu kura hiyo ipite imebadili kabisa upepo wa siasa za Zanzibar na hali imekuwa shwari mabomu ya machozi na risasi za moto na Polisi kujazana barabarani kufukuzana na wafuasi wa vyama imekuwa historia kwenye uchaguzi wa mwaka huu mpaka sasa.

SHARE
Previous article
Next article

NO COMMENTS