Mwanaharakati asema Afrika ifutiwe madeni.

0
397
Mwanaharakati  Wahu Kaara
Mwanaharakati Wahu Kaara

Mwalimu na mwanaharakati wa haki za kijamii Wahuu Kaara kutoka Kenya akiwa mjini Washington Dc hivi karibuni ambapo alitoa mada kuhusiana na kusamehewa madeni kwa nchi za Afrika.

Bi. Kaara ambaye pia ni mkurugenzi wa Kenya Debt Relief Network (KENDREN)  ambao ni washirika wa Jubilee USA  shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake hapa Washington Dc ambalo ndio liliandaa semina hiyo.

Bi Kaara  aliongelea kuhusu hali ya mgogoro wa uchumi na uchaguzi nchini Kenya akielezea umuhimu wa kusamehewa madeni na kusema nchi zilizoendelea zimechuma sana kutoka Afrika kwahiyo nchi za Afrika zisiombe kufutiwa madeni bali zidai kwani hiyo ni haki yao.

 Wakati huo huo benki ya dunia na IMF imetangaza kuifutia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo deni la dola bilioni 10, hatua ambayo imepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi wa DRC  na wanasiasa ikiwa ni kama zawadi yao kubwa wakiwa wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo mwaka huu.

SHARE
Previous articleGOLI LA PILI LA GHANA!!!
Next article

NO COMMENTS