Kibaki ailaumu jumuiya kimataifa kuhusu Somalia

0
352

Kibaki akizungumza kwenye Umoja wa kimataifa
Kibaki akizungumza kwenye Umoja wa kimataifa

Rais Mwai Kibaki amezungumza kwenye baraza la Umoja wa mataifaAlhamisi mjini New York akielezea mafanikio ya Kenya katika kufanikisha malengo ya Millenia na kupungua kwa maambukizo ya magonjwa ya Malaria, HIV na Ukimwi, vifo vya watoto wachanga na kuwapa nafasi zaidi wanawake katika jamii.

Pia Rais Kibaki alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia suala la Somalia akidai kuwa inaonekana nchi hiyo imesahaulika na jumuiya ya kimataifana kwamba suala la Somalia linaleta utete kwenye eneo zima la Afrika Mashariki na si Kenya peke yake.

Ametaka baraza kuu la Umoja wa Mataifa kutambua suala hilo na kulipa umuhimu mkubwa zaidi.

Pia Rais Kibaki akiwa na Kofia ya uenyekiti wa IGAD amesema amehusika katika kufanikisha utafutaji amani huko Sudan na akisema kwamba anawahakikishia kuwa rais wa Sudan Omar Al Bashir na makamu wake Salva Kiir wamekubali kushiriki kura ya maoni na kuahidi kuheshimu matokeo yake.

NO COMMENTS