GOLI LA PILI LA GHANA!!!

0
433
Ghana yafa kiume
Ghana yafa kiume

Wawakilishi pekee waq Afrika waliobaki kwenye kombe la dunia hawapo tena wametolewa kwa taabu kwa mikwaju ya penalti na timu ya taifa ya Uruguay. Timu hiyo ilipona baada ya mshambuliaji wake Suarez kuokoa bao la wazi kwa mkono na kuiita huo ulikua mkono wa Mungu sawa na ule wa Maradona uliokuwa mwaka 1986 ambao alifunga bao la mkono. Tofauti yake safari hii ni kwamba Suarez alizuia goli kuingia ndani ya eneo lake. Na kuacha wachambuzi wa soka wakijiuliza kwamba huu si wakati wa kuruhusu teknolojia kwenye soka.? Kwani ingekuwa hivyo mpira ule wa Ghana ungehesabiwa bao la pili baada ya kuangalia upya. Tayari rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter ametangaza mkutano ujao wa chama chake utafungua faili la kuhusiana na suala hilo.

NO COMMENTS