Benki ya dunia yaiwekea vikwazo Ivory Coast

0
304

Vikosi vya umoja wa mataifa Ivory coast Benki ya Dunia inasema imezuia fedha za Ivory Coast, ambako rais asiyetambulika aliye madarakani Laurent Gbagbo anaendelea kukumbatia madaraka licha ya kutokubaliwa na dunia nzima.

Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick alitangaza usitishaji huo wa fedha za Ivory Coast Jumatano baada ya mazungumzo na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy huko Paris.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) hatua hiyo inaongeza msukumo kwa bwana Gbagbo kukabidhi madaraka kwa mpinzani wake Alassane Ouattara, mshindi anayetambulika kimataifa katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

Mapema Jumatano, Ufaransa iliwasihi raia wake kuondoka Ivory Coast baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon kuonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

NO COMMENTS