Jumuiya ya kimataifa kumshinikiza Bgagbo

0
337

Rais aliyegoma kuachia madaraka wa Ivory Coast Laurent Bgagbo.
Umoja wa Ulaya unategemewa kuweka vikwazo dhidi ya Ivory Coast katika juhudi za kumwekea shinikizo rais wa muda mrefu, Laurent Gbagbo kukubali matokeo ya uchaguzi uliopingwa.

Kwa mujibu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA waziri wa mambo ya nje wa Finland Alexander Stubb akisema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba vikwazo vinaweza kupitishwa jumatatu katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje.

Bw. Gbagbo na mpinzani Alasane Ouattara wote kwa pamoja walidai kushinda katika uchaguzi wa hivi karibuni na wote kwa pamoja wameunda serikali zinazokinzana. Jumuiya nyingi za kimataifa ikiwa ni pamoja na baraza la usalama la umoja wa mataifa , Umoja wa Afrika na jumuiya ya uchumi ya Afrika magharibi, wanamtambua Bw. Ouattara kama rais.

Na kwa mujibu wa jarida la Times la Marekani, rais wa Marekani Barack Obama alimpigia simu rais Gbagbo lakini rais huyo aliingia mitini na kuagiza wasaidizi kusema kuwa alikuwa amelala na haukurudisha simu hiyo hata hivyo Obama ametishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

NO COMMENTS