Kuvunjika kwa ndoa ya mastaa hawa tatizo nini wanawake au wanaume?

0
408

Tony Parker na Eva Longoria enzi za mapenzi yao!
Je tatizo ni wanaume wa Hollywood na maarufu tu au wanawake pia? ndoa iliyoonekana inag’aa na kumeremeta ya Eva Longoria na Tony Parker imetangzwa kuvunjika baada ya Eva Longoria kutangaza kuchukua hatua hiyo kwa mujibu wa jarida la US Weekly.

Sasa suali linakuja pale pale tatizo nini? mume au mke maana haya yametajwa kuwa mahusiano kati ya mume wa mtu na mke wa mtu tena marafiki!! Sasa hata marafiki wasiaminiane?!

Eva Longoria na Tony Parker walikuwa pamoja kwenye ndoa muda wa miaka mitatu tu na baadhi ya marafiki zao wanasema hawakushangazwa na hilo hasa kwasababu ya umbali Tony Parker ni mcheza anayesafiri kila kona ya Marekani na mtaliki wake ni supa staa wa Desparate Housewives ambaye yuko bize kutengeneza mlolongo wa filamu hizo.

Sasa suala najiuliza je umbali ndio tatizo au ni uaminifu wa mtu tu? pengine wananchi mtanisaidia na je ni rahisi kwa wanaume au wanawake kutoka nje ya ndoa zao kukiwa na hali ya kuwa mbali na wenza wao na kama ni hivyo dawa bora ni nini?

Kwa mujibu wa US Weekly Eva aligundua mlolongo wa sms kati ya mume wake na rafiki wa kike ambaye inasemekana ni mke wa rafiki yao ambaye walicheza kikapu zamani na Tony Brent Barry aitwaye Erin Barry.

Erina alipotafutwa na US Weekly alikataa kuongea chochote lakini kuna tetesi zimeripotiwa kwamba naye moto umemuwakia mume wake anataka kumpa talaka. Kwahiyo naomba maoni yenu waheshimiwa kulikoni ndio mtindo wa kisasa au watu wafanyeje?

NO COMMENTS

  1. BIBLIA IMESEMA MWANAUME NDIO HEAD OF HOUSE HOLD SASA MWANAMKE UNAPOANZA KUTAKA KUMTUNZA MWANAUME MARA UNAJINUNULIA PETE AKUOE MARA UNAILILIA NDOA . CHAMOTO UTAKIONA