Maajabu ya Dancing with the Stars

0
417

Steven Cowan

Huyu jamaa pichani Stevem Cowan kama wamarekani wengine wengi alishtushwa sana na kushinda kwa mtoto wa Sara Palin Bristol “The Pistol” Palin aliyejipatia nafasi ya kuingia fainali za Dancing with the Stars.(DWTS) .

Bristol Plalin amekuwa akipatab maksi za chini kutoka kwa majaji wa shindano hilo lakini kwa namna fulani amekuwa akipata kura nyingi kutoka kwa watazamaji ambazo zimemuweka kwenye fainali ya michuano hiyo na kumtoa Brandy Norwood mwimbaji na mchezaji aliyeonyesha mchezo wa hali ya juu.

Baada ya kutangazwa Bristol ameingia fainali na Brandy kutolewa kwenye Tv ya abc Bw.Cowan ambaye anaishi katika jimbo la kati la Wisconsin alikwenda kuchukua bunduki yake kuijaza risasi na kufyatua risasi kadhaa kwenye runinga yake na halafu kumgeuzia kibao mkewe ambaye alikimbia na kuita Polisi ambao baadae walimkamata Bw. Cowan

Kama akikutwa na hatia Bw. Cowan anaweza kupata adhabu ya juu kufikia kifungo cha miaka 20 jela. Naye Bristol Palin alipoulizwa kwa mujibu wa jarida la People kuwa jina la mama yake na vugu vugu la Tea Party ndio wanaomfikisha hapo alipo kwa kura zao alikataa jambo hilo na kudai kwamba yeye anastahili kwani alianza akiwa hajui kabisa kucheza na sasa amejitahidi mno na kuwa na mabadiliko makubwa katika uchezaji wake.

Bristol Palin na partner wake Mark Ballas

NO COMMENTS