HIKI NDICHO KIPAJI KIPYA ALICHOKIIBUA MWANAMUZIKI SNURA KWA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA YANGA NA TAIFA STARS MRISHO HALFAN NGASSA


Mrisho Halfan Ngassa anavyo mbebeleza mahaba ya Snura kwa kumsuka nywele.

WAKATI hali ikizidi kuwa tete nyumbani kwa mshambuliaji wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa baada ya kudaiwa kuwa kumeibuka ugomvi mkubwa baina yake na mkewe.

Ugomvi huo unatokana na siri ya mahusiano ya mepenzi baina yake na Msanii wa Musiki wa Kizazi Kipya Snura Anton, maarufu kwa jina la majanga, msanii huyo amejitokeza hadharani na kudai kwamba hana mahusiano ya kimapenzi ya mwanasoka huyo.

Tangu jana picha za wawili hao zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakiwa kwenye pozi mbalimbali za mahaba huku Ngassa akigeuzwa msusi wa nywele za mwana dada huyo mwenye sifa ya kurubuni wanaume, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutumia makalio yake ipasavyo wakati wowote.

Katika maelezo yake ambayo pia yamezagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii Snura amaesema kwamba, Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo.

“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu na alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu”;

“Tatizo ni kwamba, simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo” Ngassa ambaye anaonekana kuwa msusi mahiri wakati mahaba akionyesha kila dalili za kuchanganywa na mahaba ya kimwana huyo.

Hata hivyo Habarimpya.com ilimtafuta Ngassa ambaye hivi sasa yuko kwenye kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza mechi ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) lakini akashindwa kusema lolote kwa madai kwamba hivi sasa hapaswi kuzungumza chochote juu ya suala hilo.

Mwaka 2011 akiwa katika kikosi cha Azam, Ngassa aliwahi kufumaniwa akiwa na mwanamke chumbani kwake, wakati huo akiishi katika chumba kimoja maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam, tukio hilo lilimpa fedheha mshambuliaji huyo mahiri nchini Tanzania, baada ya mkewe kupiga kelele na kualika mtaa mzima nyumbani kwake kuja kushuhudia fumanizi hilo.jumamtanda

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s