Mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akijiachia jukwaani na mmoja wa mashabiki waliyejitokeza kucheza nae,kwenye shoo ya Usiku wa Mtu mzima Dawa uliofanyika kwenye kiota cha maraha cha Villa park usiku wa kuamkia Jumamosi,jijini Mwanza.Aidha katika makamuzi hayo washabiki wapenzi wa muziki wa kizazi kipya walijaa ile mbaya na palikuwa hapatoshi hata kidogo.
Wasanii Chege na Ydash wote kutoka Wanaume TMK wakiwarusha wakazi wa Mwanza ni kibao chao cha Dar mpaka Moro.
Wanaumeeee…eeeeeh..! Wanauuumeeeee…..halafu mashabiki wanaitikia kwa nguvu kabisa eeeehhhh..!
“Sijui nimtawanyee…..aah huwezi wewe mtu mzima dawa.”! Mh Temba akikamua vilivyo na Bibi Cheka jukwaai saafi kabisa huku shangwe zikiwa zinasikika kila kona,kwani Bibi Cheka alionesha uwezo wake mkubwa wa kukamua jukwaa,hata ile mitindo huru nini na niniii yuko swafi mbaya..aaah mbona palinoga Villa Park usiku wa kuamkia Jumamosi.
Ommy Dimpoz akikamu mbele ya umati mkubwa ndani ya kiota cha maraha cha Villa Park usiku wa kuamkia Jumamosi.
Watu nyomi walifurika ndani ya ukumbi wa Villa Park kushuhudia Usiku wa mtu mzima dawa.
Pamoja na kupotea kiaina kwenye gemu ya muziki wa Bongofleva,Ferouz bado nyota yake inaonekana kuwa angavu,alifanya vyema ndani ya ukumbi wa Villa Park,kiasa kwamba shangwe kila wakati zilikuwa za kutosha.
Mkali mwingine wa mitindo huru,Mwana FA a.k.a Binadamu akikamua vilivyo ndani ya ukumbi wa Villa Park usiku wa kuamkia leo,kwenye shoo ya usiku wa mkubwa dawa ambao ulifana kwa kiasi kikubwa.Picha zote na Michuzijr.Blogspot.com
Archive for July 7, 2012
Usiku wa mtu mzima Dawa wafana Mwanza.
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday ShomariWABUNGE WA SIMBA WABAMIZA WENZAO WA YANGA KWA MATUTA 3-2
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari

Wabunge wa wa timu ya wabunge ya Simba wakishangilia baada ya kuwafunga watani wao wabunge wa Yanga kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Jumamosi.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2. Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2.
WANYARWANDA WAINGIA NA MTAMBO WA KUNYONYA SUMU MWILINI
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari
Mtambo maalum wa kuondoa sumu mwilini mwa binadamu wagundulika na wananchi wameaswa kuangalia afya zao mara kwa mara kutokana na kula vyakula vyenye kemikali ambazo hutengeneza sumu ndani ya miili yao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Dk Emmanuel Shoo katika banda la Wanyarwanda kwenye maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyrere nchinin Tanzania na kusema kwmba mwili wa binadamu unachukua sumu nyingi kutokana na vyakula vya kisasa.Kusoma zaidi bofya Read more »
HALI YA DK.ULIMBOKA MBAYA , MUHIMBILI, MOI BADO HAKUJATULIA, SERIKALI SASA YAWASHTAKI MMOJA MMOJA
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari
Mwenyekiti Jumuiya ya Madaktari Tanzania,Dk Stephen Ulimboka.
Uongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, umekiri kuwa hali ya Mwenyekiti wake, Dk Stephen Ulimboka ni mbaya na sasa amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika hospitali anakotibiwa huko Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Mwananchi taarifa za Dk Ulimboka kuwa mahututi zilianza kupatikana juzi lakini hakuna daktari yeyote aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo baada ya kila aliyekuwa akiulizwa kueleza kuwa taarifa hizo zilikuwa uvumi tu.
“Asubuhi wote tulisikia kwamba hali yake (Dk Ulimboka) ni mbaya na yuko kwenye ‘koma’, lakini taarifa hizo sijazithibitisha kujua zina ukweli kiasi gani,” alisema Kiongozi wa jopo la madaktari linaloshughulikia matibabu ya Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahama juzi huku Katibu wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila akisema alikuwa haelewi uvumi huo ulitoka wapi kwani yeye hakuwa na taarifa hizo.Kusoma zaidi bofya Read more »
HASHEEM THABIT ATUA OKLAHOMA
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari
Hatimaye nyota wa kimataifa wa mchezo wa kikapu, Hasheem Thabeet ambaye ameshindwa kung’ara kwenye Ligi ya NBA tangu aliposhika nafasi ya pili kwenye mashindano ya vyuo mwaka 2009,amepata nafasi nyingine amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu ya Oklahoma City Thunder, limeripoti gazeti la Daily Oklahoman.
Thabeet alitasaini rasmi mkataba huo mpya Julai 11 mwaka huu.Makubaliano ya mkataba huo hayajawekwa wazi, lakini taarifa zinasema kuwa ni mkataba wa kudumu wa misimu yote miwili.
Kwa mujibu wa Oklahoman, Thabeet atalipwa mshahara wa dola 880,000 (Sh1.3 Bilioni) katika mwaka wake wa kwanza wa mkataba.
Gazeti hilo limeeleza kwamba, mshahara huyo ni mdogo zaidi kulipwa kwenye ligi.Thabeet mwenye urefu wa futi 7.3, anajiunga na timu hiyo mpya, ikiwa ni ya nne kwake katika misimu minne ya kucheza tangu mwaka 2009.
James Harden, Tyreke Evans, Stephen Curry, Jrue Holiday, Brandon Jennings na Ricky Rubio ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa toka kwenye mashindano ya vyuo baada ya Thabeet mwaka 2009.Akiwa amecheza michezo 135 ya Ligi Kuu ya Kipapu Marekani (NBA), Thabeet ana wastani wa pointi 2.2 ya kucheza mipira inayorudi na pointi 0.9 ya kuzuia.
Wastani huo ni sawa pointi 1.8 na 2.1 kwa mipira inayorudi katika mechi 20, lakini kwa zile tano ya mwisho akiwa na timu ya Houston, na michezo 15 akiwa na timu ya Portland.
RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI DODOMA
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi serikalini baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.
PICHA NA IKULU
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KUDUMU WA TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC (DMV)
Posted in Uncategorized on July 7, 2012 by sunday Shomari
Tunapenda kuwatangazia wanachama wote wa Chadema Tawi la Washington DC (DMV) kuwa Tarehe 15 July 2012 siku ya Jumapili, tutafanya uchaguzi wa Viongozi wa kudumu wa Tawi ambao watachukua nafasi za waliokuwa Viongozi wa Muda.
Nafasi zitakazogombewa
Mwenyekiti wa Tawi
Katibu wa Tawi
Katibu Mwenezi
Mweka hazina
Mjumbe wa Vijana
Mjumbe wa Wanawake
Tuma maombi yako na nafasi unayotaka kugombea kwa kuandika majina matatu, Namba yako ya simu na email kwenda kwenye email chademausa@gmail.com
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Ijumaa
13 July 2012
Ukumbi utakapofanyika Mkutano tutawajulisha Ijumaa 13 July 2012
Asanteni
******




