Archive for July 2, 2012

MSEMAJI WA MBUNGE HOWARD BERMAN AONGEA NA VOA JUU YA MATUMIZI YA BENDERA YA TANZANIA KWENYE MELI ZA IRAN

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari

Mahojiano ya VOA na msemaji wa Mbunge wa Marekani Howard Berman aliyeandika barua kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete kuhusiana na matumizi ya bendera ya Tanzania kwenye meli za Iran na maelezo ya naibu waziri wa miundo mbinu na mawasiliano wa Zanzibar akieleza meli hizo ni za Uingereza na si Iran. Kusikilkiza bofya hapa.


Warembo Mis Universe watembelea TGNP

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Wasanii warembo na wanamitindo wa Tanzania wametakiwa kuunganisha nguvu zao na kudai haki zao hussan ya kupata kipato stahiki kinachoendana na hadhi yao wanaposhiriki maonyesho, kutengeneza matangazo au sinema.

Akizungumza wakati warembo hao walipofanya ziara ya kujifunza, (study tour) TGNP, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya, amesema kuwa bado wasichana na wanawake walioko kwenye urembo wameendelea kuchukuliwa vibaya na vyombo vya habari na kukiuka maadli, ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto umendelea na mfumo umeshindwa kuthibiti wa wasichana wasitumike vibaya.

“Wasichana wanatumika vibaya, wanatendewa ukatili mkubwa, hakuna usawa katika mgawanyo wa rasilimali hasa malipo, suala kubwa ni kuhakikisha tunanufaika sawa katika rasilimali zetu kuanzia ngazi ya familia, hadi Taifa na kuunganisha nguvu ya pamoja’ amesema Mallya.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilaino TGNP, Lilian Liundi, amesema kuwa warembo na wasanii hata wanamitindo wanapaswa kujitambua kwa kujiwekea viwango vya malipo kwa kazi zao. Kusoma zaidi bofya Read more »

MADAKTARI MUHIMBILI WAREJEA KAZINI

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.

Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.

Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo

Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.

Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..

KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.

Imetolewa na;

Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 1, 2012

Nitapigania wanyonge hadi pumzi ya mwisho-Sitta.

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema hawezi kuvumilia vitendo vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiomjua Mungu na kwamba ataendelea kupigania haki za wanyonge hadi pumzi yake ya mwisho.

Waziri Sitta aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Anglikana la Matakatifu Andrew Magomeni jijini Dar es Salaam.

Alisema viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu kutenda mambo mema katika jamii lakini bado kumekuwa na vitendo vya kinyama, rushwa, ubaguzi ambavyo vinafanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya watanzania.Kusoma zaidi bofya Read more »

MWANADIASPORA KHAMSIN IDDI ALKHAG ALONGA NA VIJIMAMBO SEHEMU YA II

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari

Maoni ya Mbunge wa Ubungo kuhusu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Tanzania

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari

Julai 2012 kumesambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari hotuba ya Mh. Dkt. Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi inayotajwa kutolewa tarehe 30 Juni 2012.


Kufuatia hotuba hiyo na kufuatia mwito kutoka wachangiaji wa mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kutaka maoni yangu kuhusu hotuba husika, naomba nichukue fursa hii kutoa maoni kwa nafasi yangu ya ubunge kuhusu hotuba tajwa kama ifuatavyo:

Hotuba hiyo ya Rais imeibua mjadala na masuala ambayo yanahitaji kujadiliwa bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge unaoendelea hivyo, serikali isiendelee tena kutumia kisingizio cha mahakama kulizua bunge kujadili masuala husika wakati yenyewe inayajadili na kuyatolea maelezo na maelekezo pamoja na kuchukua hatua hususani kuhusu suala la mgomo wa madaktari.

Hotuba hiyo ya Rais ukindoa suala la usafirishaji haramu wa watu nchini inaelekea kuwa ndiyo kauli ya Serikali ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kwamba ingetolewa bungeni lakini baadaye serikali ikasema haitatoa kauli. Uamuzi wa Serikali kuitoa kauli hiyo kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge wasijadili hotuba husika na pia wasitimize wajibu wa kikatiba wa ibara 63 (2) wa kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi. Kusoma zaidi bofya Read more »

Tanzania yashutumiwa kuruhusu meli za Iran kutumia bendera yake.

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Tanzania imetakiwa kusimamisha matumizi ya bendera yake katika meli za mafuta za Iran ikiwa kama juhudi za nchi hiyo kukwepa vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Mbunge mwandamizi katika baraza la wawakilishi la bunge la Marekani, Howard Berman, mdemokrat kutoka California amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kumtaka asimamishe matumizi ya bendera ya Tanzania katika meli za Iran baada ya ripoti kuwa meli za kampuni ya usafirishaji mafuta ya Iran, NITC, zimesajiliwa kama meli za Tanzania na kupeperusha bendera ya nchi hiyo.

Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano wa Zanzibar Issa Haji Gavu amesema katika mahojiano na Sauti ya Amerika, VOA, kuwa meli hizo zilisajiliwa Zanzibar kama meli za Uingereza sio meli za Iran.

Mbunge Berman amesema katika barua hiyo ya Juni 29 kuwa misaada ya Marekani kwa Tanzania itakuwa hatarini endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Katika barua hiyo Berman anasema “inasikitisha sana kuona kuwa serikali yako imechukua hatua zinazokiuka ushirika wa kimataifa unaoshirikiana, kwa njia za amani, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya uchumi, kubadili mwenendo hatari wa serikali ya Iran. Uamuzi wa kuruhusu NITC kutumia bendera ya Tanzania unatilia mashaka sifa za Tanzania kimataifa.”

Tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka saba iliyopita Tanzania imekuwa ikipata misaada mikubwa kutoka Marekani katika mpango wa afya wa PEPFAR ulioanzishwa na Rais George Bush na mpango wa Millenium Challenge unaoshirikiana na nchi zinazoonyesha maendeleo duniani.Kusikiliza mahojiano na Naibu waziri Issa Hajji Gavu bofya hapa.


Obama alaani mashambulizi ya Garissa

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Marekani imelaani vikali mashambulizi ya Jumapili katika makanisa mawili huko Garissa, Kenya na kuuwa watu wapatao 17 huku wengine zaidi ya 40 wakiwa wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa VOA mashambulizi hayo ya Garissa yametokea siku chache kufuatia kuuawa kwa mfanyakazi mmoja wa misaada na kutekwa kwa wengine wanne kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab, na kabla ya hapo kulitokea shambulizi katika klabu moja ya starehe mjini Mombasa wiki iliyopita.

Taarifa ya White House iliyotolewa Washington Jumapili jioni ilisema watu waliofanya mashambulizi hayo hawakuonyesha heshima yoyote kwa maisha ya binadamu, na ni lazima wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria mapema iwezekanavyo.

Hatuhusiki unyama aliofanyiwa Ulimboka -JK

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari

Rais Jakaya Kikwete
ASEMA MADAKTARI WASIOKUBALI MSHAHARA WA SERIKALI WAFUNGASHE VIRAGO

Wakati Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiendelea na matibabu Afrika Kusini, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali haihusiki na kilichomtokea daktari huyo kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu katika majadiliano baina ya pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa Mwananchi Rais Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kila mwezi, ambapo mbali na suala hilo, pia alizungumzia sababu za mgomo wa madaktari na usafirishaji wa wahamiaji haramu.Kusoma zaidi bofya Read more »

Rais Kikwete na mama Salma wahudhuria miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda

Posted in Uncategorized on July 2, 2012 by sunday Shomari


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakipokea heshima za marais muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda Jumapili asubuhi.
Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali Rwanda kwa ajili ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Rwanda.(Picha na Freddy Maro)

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,726 other followers