Archive for May 26, 2012

Pepe Ndombe afariki kutokana na mshtuko wa moyo

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari


Ndombe Opetum maarufu ya Pepe alianza muziki akiwa na umri wa miaka 18, alianzia kwenye bendi ya Afrikan Fiesta ya Pascal Rochereau Tabu Ley.

Ndombe Opetum alijipatia umaarufu baada ya kuondoka kwenye bendi hiyo ya African Fiesta kwa wanamuziki Sam Mangwana, Mavutico na wengine .

Pepe Ndombe ameacha kibao kipya cha muziki ambacho ametoka kurikodi.Mwanamuzi Adolphe Do Minguez ambae nilimkuta kwenye studio ya kurikodi nyimbo amelezea ujasiri wa Pepe Ndombe

Wizara ya utamaduni na sanaa imepanga kumuandalia maziko ya heshima mwanamuziki huyo ambae mwanae Baby Ndombe amefuata nyoyo za babake nakuwa mwanamuziki chipukizi hapa nchini.

Pepe Ndombe anatarajiwa kuzikwa wiki ijayo.

MAHOJIANO NA ZITTO PART 4

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

MAHOJIANO NA ZITTO PART 3

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

MAHOJIANO PART 2

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

MAHOJIANO NA ZITTO KABWE PART 1

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

Mbunge wa Kigoma kaskazini na naibu kiongozi wa upinzani bungeni na naibu katibu mkuu wa Chadema alizungumza na Mubelwa Bandio wa Changamoto yetu blog spot.com

MEMORIAL WEEKEND COLUMBUS OHIO MAMBO NDIO YAMEANZA

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

Wakazi wa Columbus Ohio katika African Flava.
Kulia Frank Kambira a.k.a Mr Prezida akiwa na wadau wengine wa Nc na Columbus katika Afrikan Flava.
Dimo a.k.a Dimo D akiwa na Pamela a.k.a Pam Lolo. katika Afrikan Nite.
Bw na Bi Akili Lusungu a.k.a Mtalaam wakila pozi.
Mr.Gonga akila pozi la Gonga.
kwa picha zaidi Read more »

STEVE NYERERE AGAWA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KINONDONI.

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

Stevin Mengele ‘Steve Nyerer’ akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Ijumaa kwa ajili ya kutambulisha filamu yake ya Nyerere.
 Msanii Stevin Mangele katikati akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps Pritesh Chavda na Mwandishi wa habari wa kituo cha EATV Patrick Nyembela wakati alipokwenda kutembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa Zawadi ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya ‘Nyerere’ Ijumaa.
Stevin Mengele ‘Steve Nyerere’ katikati akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Maunga Kinondoni Dar es salaam Ijumaa.(Picha kwa hisani ya Hakingwi).

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDO MBINU YATEMBELEA MIRADI MKOANI RUKWA

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

BB Mhe. Shekifu na Kamati yake wakiangalia moja ya eneo lililoanza kupata nyufa katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami. Mwenyekiti huyo alimuasa Mkandarasi huyo mambo matatu moja ikiwa ni kupata taarifa rasmi yenye uhakika kutoka kwao kuwa ni lini mradi huo utakamilika ili wawatangazie wananchi wenye kiu kubwa na barabara hizo. Pili wahakikishe ubora wa barabara hizo unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyowekwa lami. Na mwisho ni kuhakikisha suala la fidia kwa wananchi wanaostahiki linakamilika kuepusha usumbufu wowote ule.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu wa tatu kushoto Meneja wa Tanroad Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka na wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Bunge wakishika udongo uliochanganywa na Cement na kushindiliwa ikiwa ni mojawapo ya hatua kuelekea ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara ya Laela Sumbawanga eneo la kyanda walipokagua ujenzi wa barabara hiyo.(Picha na Habari na Hamza Temba-Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Rukwa.)

MBUNGE WA ROMBO MH.JOSEPH SELASINI APATA AJALI MBAYA

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

Mbunge wa Rombo(CHADEMA), Mhe. Joseph Selasini.

Mbunge wa Rombo(CHADEMA), Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza maisha na miili yao imechukuliwa na gari la polisi na kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kutoka Boma Ng’ombe.

Ajali hiyo imetokea wakati gari alilokuwa akiliendesha kupasuka tairi la mbele na kupinduka eneo la darajani. Taarifa za awali zinasema kuwa watu watatu kati ya Watano waliokuwemo kwenye gari hilo wamefariki Dunia hapo hapo – akiwemo Mama yake Mzazi na Shangazi yake!

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo akielezea zaidi amesema ilikuwa ni saa 1:00 jioni maeneo ya Boma Ng;ombe ambapo Mh Joseph Selasini wakati akiendesha gari hilo akitokea Arusha, ghafla aliona mwendesha Pikipiki wakati akijaribu kumkwepa ndipo gari lake likapinduka.

Watu wengine akiwemo mbunge huyo na mke wake alifahamika kwa jina la Digna Kavishe waliojeruhiwa katika ajali hiyo, wako katika hospitali ya Boma Ng’ombe hali zao zinaendelea vizuri na muda mfupi nao watapelekwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.

Kwa hisani ya HakiNgowiblogspot

WAFUASI WA CHADEMA WALIVYOSHEHEREKEA USHINDI WA MAHAKAMANI

Posted in Uncategorized on May 26, 2012 by sunday Shomari

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akipeana mkono na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Wafuasi wa Chadema nyomi mahakamani.
Mfuasi wa Chadema akitoka kwa furaha mahakamani.
Waliokuwa mitaani nao walilipuka.
Kazi ipo.
Wafuasi wa CCM waliokuwa mahakamani hapo wakiwa wameshikwa na masikitiko.
(Picha kwa hisani ya Haki Ngowi).

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,708 other followers