Archive for May 16, 2012

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MKOA WA MTWARA

Posted in Uncategorized on May 16, 2012 by sunday Shomari


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo huku wakishuhudiwa na Meneja wa Mahusiano Bi. Shy-Rose Bhanji wakati wa kukabidhiwa msaada wa Madawati kwa Shule za Mkoa wa Mtwara.
(Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara)

RAIS DKT.SHEIN AFANYA UTEUZI ZANZIBAR

Posted in Uncategorized on May 16, 2012 by sunday Shomari


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohd Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Mdungi Makame Mdungi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.

Aidha Dkt. Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amemteuwa Khamis Jabir Makame kuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 16 Mei 2012,

KEKI YA BIRTHDAY YA VOA SWAHILI

Posted in Uncategorized on May 16, 2012 by sunday Shomari

Mtuu mmoja akamatwa kutokana na shambulizi la bomu Mombasa.

Posted in Uncategorized on May 16, 2012 by sunday Shomari

Polisi mjini Mombasa imemkamata mtu mmoja mshukiwa wa ugaidi, anayehusishwa na shambulio la Grunedi katika Mgahawa mmoja maarufu katika mji huo.

Shambulio hilo la Jumanne usiku katika ukumbi wa CLUB BELLA VISTA, lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Kwa mujibu wa VOA mshukiwa huyo amekuwa akihudumia majeraha aliyopata kutokana na shambulio hilo katika hospitali moja mjini Mombasa na majeruhi wengine watano. Washukiwa wenzake wamefanikiwa kutoroka.

Mtu huyo aliyefariki ni mfanyakazi wa club hiyo ya Bellavista inaripotiwa kuwa watu watatu wenye silaha walivamia mgahawa huo wakiwa na vifaa vya vilipuzi na bunduki.

Baada ya kukaidi amri ya kukaguliwa na walinzi wa mgahawa huo walirusha guruneti na kufyatua risasi kwenye mgahawa huo maarufu kwa kuonyesha michuano ya kandanda ambao huvutia watalii na raia wa Kenya.

Hili ni shambulio la tatu chini ya miezi mitatu mpaka sasa zaidi ya watu 10 wamefariki dunia katika visa tofauti tangu jeshi la Kenya kuingia Somalia katika jitihada za kuwasaka Al shabab.
Akizungumza na Sauiti ya Amerika kiongozi wa jumuiya ya kiislam nchini Kenya shekhe Mohamed Door amesema ni idadi ya kikosi cha polisi ni ndogo sana na lazima serikali iongeze idadi ya Polisi , vituo vya polisi na magari akiongeza hilo si ombi bali ni jukumu lao.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,707 other followers