Archive for May 10, 2012

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA MITAJI NA MAZAO LA ETHIOPIA

Posted in Uncategorized on May 10, 2012 by sunday Shomari


Rais Jakaya Kikwete akipinga kengele kuashiria kuanza kwa soko katika makao makuu ya soko la hisa na mitaji ya mazao la Ethiopia Alhamisi wakati alipotembelea na kuelezwa mafanikio ya soko hilo ambapo wakulinma wakubwa na wa kawaida wanafanya biashara ya mazao kitaifa na kimataifa kwa nia ya kisasa. (Picha kwa hisani ya Michuzi).

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI

Posted in Uncategorized on May 10, 2012 by sunday Shomari

Ujumbe wa Majaji naMahakimu kutoka Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja, mara baada ya kukabidhiwa rasmi Bango la Chama hicho cha Majaji Duniani(AIWJ)nakupewa nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu ujao wa Chama hicho utakofanyika Mwezi Mei, 2014 Mjini Arusha – Tanzania.

Chama cha Majaji Wanawake duniani (IAWJ) kilikuwa na mkutano wake Mkuu uliofanyika London Uingereza tarehe 2-5 Mei 2012.

Kwenye Mkutano huo Tanzania,iliwakilishwa na Majaji na Mahakimu ambao ni wanachama wa IAWJ (International Association of Women Judges) na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA).Kusoma zaidi bofya Read more »

Membe: Bado sijaoteshwa Urais 2015

Posted in Uncategorized on May 10, 2012 by sunday Shomari


Katika kionekanacho kuwa kinyang’anyiro cha viongozi wengi wa Tanzania kutangaza kuwania urais 2015, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hajaoteshwa kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.

Viongozi wengi na wabunge aidha wametangaza nia zao au kuonyesha nia ya wazi kwenye mbio hizo ungana na gazeti la Mwananchi kwa yale yaliyo moyoni mwa waziri Bernard Membe.

Akizungumza Dar es Salaam Jumanne na Mwananchi, Waziri Membe alisema harakati za kugombea urais siyo kitu kidogo cha kukurupuka, kwani unatakiwa kuwa na muono unaokujia kuwa mgombea.Kusoma zaidi bofya Read more »

NDEGE MPYA YA ATCL KUWASILI

Posted in Uncategorized on May 10, 2012 by sunday Shomari

Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limepata ndege nyingine aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili alhamisi Mchana (kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo Jumatano ilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi huo.Kusoma zaidi bofya Read more »

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,704 other followers