Archive for May 2, 2012

DR.MAKONGORO MAHANGA ASHINDA KESI.

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari

Mbunge wa jimbo la Segerea (CCM) na naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga akilakiwa na wafuasi wa wake baada ya kuibuka kidedea katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo iliyokuwa inamkabili katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Fredi Mpendazoe.
(PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE)

TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA YAKABIGHIWA OFISI

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari

Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza , wa pili kutoka kushotoni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba na Angela Kairuki mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam.(Kwa hisani ya FullShangwe).

LINAH NDANI YA NY-TAMANI TOUR.

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari

Semina ya Neno la Mungu na Christopher Mwakasege May 24 2012

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari

HATIMAYE GINGRICH AACHIA NGAZI

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari


Mgombea urais wa chama cha Republikan Newt Gingrich amewaambia waunga mkono wake kwamba anajitoa kwenye kinyang’anyiro cha urais siku moja kabla ya kutangaza rasmi.

Kwa mujibu wa VOA Gingrich aliweka video kwenye mtandao wake na kuwashukuru karibu watu laki moja na themanini ambao walichangia kampeni yake na karibnu milioni 2 na nusu waliompigia kura katika uchaguzi wa uteuzi wa chama cha republican.

Bila kumtaja Mitt Romney mgombea mtarajiwa wa chama cha Republikan , Gingrich alisema nchi bado inapambana na mzozo mkubwa na kusema kuchaguliwa tena kwa rais Barack Obama wa chama cha democrat itakuwa ni janga la wazi.

BOKO HARAM WAITOLEA VITISHO VOA

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari


Kundi moja la wanamgambo limewatishia mashirika kadhaa ya kimataifa na ya nyumbani ikiwa ni pamoja na idhaa ya Hausa ya Sauti ya Amerika.

Kwa mujibu wa VOA vitisho hivyo viko kwenye video ya dakika 18 kwenye mtandao wa You tube Jumanne kwa jina la kundi la kiislam la Boko Haram.

Video hiyo inaonyesha gari ikilipuka mjini Abuja Alhamisi nje ya jengo la This Day moja ya gazeti mashuhuri la taifa.

Waandishi wa habari Iringa kutumia siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kumweka kiti moto mbunge Msigwa

Posted in Uncategorized on May 2, 2012 by sunday Shomari


Na Francis Godwin, Iringa.
Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo duniani .

Alisema kuwa mdahalo huu katika ya wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote kufika.Kusoma zaidi bofya Read more »

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,705 other followers