Archive for May 1, 2012

Stock Market Newsletter: “SELL IN MAY…AND GO AWAY”

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

David Magness-
This OLD STOCK MARKET CLICHE’ has been around since the 1950′s…The STOCK TRADER’S ALMANAC says that for the last 50+ years…this AXIOM has been TRUE about 75% of the TIME…

…Last year [2011]…the DOW PEAKED at 12,876.00 on MAY 2ND…the STOCK MARKET then FELL 2471.51 POINTS to the LOW for the YEAR of 10,404.49…on OCTOBER 4TH…["Sell In May...& Go Away"]

…but this is an ELECTION YEAR…and ELECTION YEARS are VERY UNPREDICTABLE…but we will TRY ANYWAY…

…ALMOST without EXCEPTION…the markets DROP the FIRST WEEK in MAY…so we EXPECT A MAJOR DROP this COMING WEEK…but after that…we believe the BULL MARKET STILL has some distance to GO…before TURNING DOWN…Our PROJECTIONS indicate a MARKET TOP between MAY 15TH and MID JUNE…The LAST DAYS of a BULL MARKET cycle…are USUALLY RAPID and CHAOTIC…

…SUMMARY…We EXPECT A STOCK MARKET DROP THIS COMING WEEK…BUT then…A Trading OPPORTUNITY…TRADERS should therefore…SELL MONDAY and WAIT for this BUYING OPPORTUNITY…to appear…PROBABLY sometime LATER NEXT WEEK…or as EARLY as the END OF THIS WEEK…

…TSP PARTICIPANTS…Should REMAIN in the C FUND…

DANIEL NYALUSI ALONGA NA VIJIMAMBO

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

TUNDU LISSU AUNGURUMA SINGIDA BAADA YA KUSHINDA KESI

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

Mbunge wa Singida mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano.
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack.(Picha kwa hisani ya H@ki Ngowi).

Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.

Mnadhimu mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida, kwa lengo la kukiimarisha chama, baada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.Kusoma zaidi bofya Read more »

Kesi ya Mahalu:Mkapa Kortini Mei 8

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari


Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 8, mwaka huu kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu.Wakili anayemtetea Balozi Mahalu, Mabere Marando alisema Jumatatu kwamba Mkapa atapanda kizimbani siku moja baada ya Profesa Mahalu kumaliza kutoa utetezi wake.

Kwa mujibu wa Mwananchi awali, akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilvin Mgeta Wakili Marando alisema Mei 8, kutakuwa na shahidi mwingine wa mwisho muhimu ambaye hata hivyo, hakumtaja.Kusoma zaidi bofya Read more »

CCM yapoteza kiti cha ubunge Sumbawanga

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

Aliyekua Mbunge wa Sumbawanga Mjini(CCM)Aeshi Hillary.

Aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM) Aeshi Hillary amevuliwa ubunge na mahakama, kufuati hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Sumbawanga Mjini dhidi ya Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye alidai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Miongoni mwa madai mengine ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki n.k.
CHANZO:H@ki Ngowi blog

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

Wanachama wa CUF wakimshangilia Rais Kikwete mjini Tanga.(Picha na Ikulu).
Wafanyakazi nchini Tanzania leo wanaungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi), huku wakieleza kilio chao kuwa ni ukubwa wa viwango vya kodi ya mapato (PAYE) na kiwango kidogo cha mishahara ikilinganishwa na ongezeko la mfumuko wa bei.

Kwa mujibu wa Mwananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti Jumatatu walisema watapeleka kilio hicho kwa Rais Jakaya Kikwete Jumanne katika maadhimisho ya sherehe hizo ambazo yeye atakuwa mgeni rasmi. Maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi yanafanyika kitaifa mjini Tanga.Kusoma zaidi bofya Read more »

RAIS KIKWETE APOKELEWA KWA SHANGWE TANGA

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Nicholaus Mgaya Jumatatu April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi.(Picha na Ikulu).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya masista na mapadre kati ya mamia ya wakazi wa jiji la Tanga Jumatatu baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikweteakiwapungia mkono mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga ba pia wanachama wa CUF Jumatatu April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakazi wa jiji la Tanga wengi wao wanachama wa CUF wakiwa na bendera na kuonyesha tofauti za vyama si uadui.

Kiraithe: Kenya iko salama

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari


Polisi nchini Kenya wanaendelea na uchunguzi wa mripuko uulotokea katika kanisa la “God’s House of Miricales International” Jumapili, lililosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 16 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa VOA msemaji wa polisi Eric Kiraithe ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wanauhakika katika muda wa saa 48 hadi 72 wataweza kumtambua aliyehusika na shambulio hilo lililotokea wakatti waumini walikua wanahudhuria misa ya Jumapili.

Tuko na fununu, lakini kama amefadhiliwa na kundi hili au lingine baado hatujapata mwangaza.Tuko na mshukiwa lakini hatuna hakika kuhusu mambo mengi kuhusiana nae. Tuna fununu juu ya hasa yeye ni nani.”

Waathiriwa wamelaani kitendo hicho, na madaktari wa Kenyatta Hospital wanasema watu 9 kati ya walolazwa hospitali wako katika hali nzuri.

Maafisa wa serikali wamewatembelea waathiriwa, hospitali akiwemo Makamu rais Kalonzo Musyoka ambae amelaani kitendo hicho akikieleza kuwa ni ugaidi, na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

MKUTANO WA JOEL OSTEEN DC NYOMI

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari

Baadhi ya umati wa waumini waliofurika katika mkutano wa Joel Osteen mchungaji maarufu Marekani alipotembelea jiji la Washington Dc, mkutano huo ulikuwa ufanyike Jumamosi lakini uliahirishwa na kufanyika Jumapili kutokana na mvua. (Picha na ripota wetu Dc).

White house yajibu ukosoaji kuhusu kuuwawa Bin Laden

Posted in Uncategorized on May 1, 2012 by sunday Shomari


Rais wa Marekani Barack Obama anasema utawala wake hauingizi siasa kwenye mashambulizi yaliomuuwa Osama Bin Laden , na kupinga ukosoaji kwamba White house inajitumbukiza katika kusheherekea kupita kiasi juu ya kifo cha kiongozi huyo wa ugaidi.

Kwa mujibu wa VOA akizungumza siku kadhaa kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu mashambulizi ya makomandoo yaliomuuwa kiongozi wa Alqaeda Osama Bin Laden, Bw.Obama alisema jumatatu kuwa kuna wengine ikiwa ni anaonyesha wazi kumlenga mpinzani wake katika uchaguzi wa Novemba ambao wamebadili misimamo yao juu ya kufanya jambo kama hilo.

Bila kumtaja Romney kwa jina Bw.Obama alipendekeza kuangalia maelezo ya siku za nyuma ya watu juu ya suala hilo. Romney alisema miaka kadhaa iliyopita kuwa haikuwa na maana yeyote kutumia fedha nyingi kumfuatilia mtu mmoja, lakini Jumatatu alisema kuwa angeagiza Bin Laden auwawe.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,704 other followers