Archive for May, 2012

KIKAO JUU YA HALI YA MTANZANIA ALIYEKO HOSPITALI DC

Posted in Uncategorized on May 31, 2012 by sunday Shomari

Juma lililopita, Katibu wa Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC na vitongoji vyake alitoa taarifa HII kuhusu hali ya mTanzania mwenzetu na ndugu yetu, Bwana Domitian Rutakyamirwa aliyelazwa chumba namba 523 katika hospitali ya Chuo Kikuu cha George Washington iliyopo 900 23rd St., NW. Washington, DC 20037.

Bado hali ya ndugu Domi (kama anavyofahamika kwa wengi) siyo nzuri hivyo maombi pamoja na dua vyahitajika ili Mwenyezi Mungu aweze kumuangazia.

Pamoja na maombi, leo hii, familia ya Ndg Domi itakutana na ndugu, jamaa na marafiki kujadili masuala kadhaa kuhusu hali yake.
Unakaribishwa kuhudhuria na kutoa mchango wako wa mawazo katika yale yatakayojadiliwa.

Kikao kitafanyika saa moja kamili jioni.

Anwani ni

10110 Greenbelt Rd,

Lanham,MD,20706

NYOTE MNAKARIBISHWA

Unaweza kuwasiliana na
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
Mubelwa Bandio: 240-281-0574

Wawekezaji wa shirika la nyumba lo taifa wakutana na balozi wa Tanzania Marekani

Posted in Uncategorized on May 30, 2012 by sunday Shomari


Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar, pamoja na Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka walipokutana na uongozi mzima na wawekezaji wa Shirika la Nyumba La Taifa (NHC) ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC.


Vile vile Jopo hilo litakukutana na wana Jumuia ya waTanzania waishio DMV siku ya Ijumaa June 1, 2012 kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani, Kuzungumzia utaratibu mzima wa suala la mikopo ya nyumba (Tanzania Mortgage Refinance Company) ili Mtanzania aliekuwepo njee ya nchi nae kufaidika na mradi huo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
(Picha Maelezo na Swahilivilla.blogspot.com)

WABUNGE NA VIONGOZI WA CHADEMA DMV WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA

Posted in Uncategorized on May 30, 2012 by sunday Shomari

Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) watembelea rasmi Ubalozi wa Tanzania Marekani.

Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mh. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wa pili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), wakiwa na Kaimu Balozi Mh. Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Marekani. (Kwa hisani ya Swahilivilla).Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)

Posted in Uncategorized on May 30, 2012 by sunday Shomari

MATEMBEZI VOA

Posted in Uncategorized on May 30, 2012 by sunday Shomari

Padre George Damball Paroko wa Magugu katika jimbo la Mbulu alipotembelea VOA.
Baracka Daudi akipata wasaa wa kung’aa VOA.
Baracka Daudi kushoto na Padre George Damball ndani ya studio za VOA.
Padre George akifanya mahojiano ndani ya studios.
Padre George Damball ndani ya studios.
Baracka Daudi ndani ya studioz.

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA

Posted in Uncategorized on May 30, 2012 by sunday Shomari


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
PICHA NA IKULU.

Idd Simba kizimbani

Posted in Uncategorized on May 29, 2012 by sunday Shomari


Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manane, likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh2.4 bilioni.Mbali na Simba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, washtakiwa wengine ni Meneja Mkuu wa Uda, Victor Milanzi na Mkurugenzi wake Salim Mwaking’inda ambaye pia aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza (CCM).

Kwa mujibu wa Mwananchi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincoln kumaliza kuwasomea mashtaka yanayowakabili, aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na wanaomba kesi ipangiwe tarehe ya kutajwa kabla ya kupangiwa tarehe ya maelezo ya awali. Wakili Said El- Maamry anayemtetea Simba na mwenzake, Alex Mgongolwa waliiomba Mahakama impatie dhamana mteja wao hoja ambayo haikuwa na pingamizi kutoka kwa Lincoln ambaye alisema mashtaka yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika.

Ili kujidhamini, Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta aliwataka washtakiwa kutoa hati ya nyumba na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja wao asaini bondi ya Sh500 milioni.Kusoma zaidi bofya Read more »

LADY GAGA MARUFUKU INDONESIA

Posted in Uncategorized on May 29, 2012 by sunday Shomari

Mapromota wa mwimbaji wa Marekani Lady Gaga wamesema jumapili kuwa onyesho lake la Juni 3 huko Indonesia limefutwa baada ya waislam wenye msimamo mkali kutishia kufanya ghasia kama akifanya onyesho.

Kwa mujibu wa VOA wakili wa promosheni za maonyesho Minola Sebayang amesema kuzuiwa huko si tu kwasababu ya usalama wa onyesho la Lady Gaga lakini pia kwa watu wataokuwa wakimwangalia.

Polisi wa Indonesia wamekataa kutoa vibali muhimu mpaka akubali kupunguza makali. Kundo la Islamic Defenders Front au FPI limetishia kupeleka wanachama wake 30,000 ili kumzuia Lady Gaga kutoka kwenye ndege.

KIKOSI CHA JE NIFANYEJE -VOA DARESSALAAM

Posted in Uncategorized on May 28, 2012 by sunday Shomari

Kikosi cha Je Nifanyeje Rahab Fungo, Mensiah John na Diana Damian.

MAAMUZI YA KESI YA LULU KUJULIKANA JUNI 16

Posted in Uncategorized on May 28, 2012 by sunday Shomari

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.Kusoma zaidi bofya Read more »

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,707 other followers