Archive | April 2012

Miss Ukonga na miss Tabata wafanya mazoezi ya pamoja.

Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati walipofanya mazoezi ya pamoja jana.

Warembo wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani ya urembo.

Warembo wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.
Vitongoji vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania 2012.
Wakizungumza jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.
“Tunawashukuiru sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.
Nae Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na kufnya nao mazoezi ya pamoja.
Mapema Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.
Shindano la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.
Kwa hisani ya Fullshangwe.

Shambulizi la gruneti lauwa Nairobi


Polisi nchini Kenya wanasema shambulizi la guruneti kwenye Kanisa moja jijini Nairobi limeuwa mtu mmoja Jumapili na kuwajeruhi vibaya wengine zaidi ya 10. Mpaka sasa hakuna aliyedai kufanya shambulizi hilo katika Kanisa hilo linalojulikana kama God’s House of Miracle International church lililoko katika mji mkuu wa Kenya.

Kwa mujibu wa VOA Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika siku 6 baada ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya kuonya juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi mjini Nairobi. Ubalozi huo ulitoa ujumbe huo ukionya raia wa Marekani kutahadhari.

Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na majengo mashuhuri ya serikali mjini Nairobi yakashambuliwa na magaidi. Aidha taarifa hiyo ya ubalozi ilisema wakati mahsusi wa shambulizi hilo hujulikani lakini yaaminika wanaopanga shambulizi hilo wamo katika hatua za mwisho.

JK KUBWAGA MAWAZIRI WENGI WA ZAMANI,SURA MPYA ZATABIRIWA


Wakati mawaziri wanaounda Serikali ya Awamu ya Nne wakiendelea kupata usingizi wa mang’amung’amu kwa hofu ya kupanguliwa, kuna taarifa kwamba idadi kubwa ya mawaziri wa zamani wataachwa na sura mpya hususan vijana kutawala baraza jipya.

Kwa mujibu wa Mwananchi joto la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri limeshika kasi baada ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam juzi na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa chama hicho, kuwataka mawaziri wanaoandamwa na kashfa mbalimbali katika wizara zao, kuachia ngazi.

Taarifa ya Rais Kikwete kutaka kusuka upya Baraza la Mawaziri ilitangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizikia kwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CCM.

Vyanzo vya Mwananchi vimeeleza kuwa mbali na Rais kutumia kigezo cha udhaifu uliobainishwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), atawaengua pia wale wanaoshindwa kuwajibika na wale wenye kasi ndogo ya uongozi. Kusoma zaidi bofya Continue reading

Semina ya Uamsho Columbus, OH

Tunawakaribisha wote kwenye Semina ya Uamsho itakayofanyika hapa Columbus, Ohio wiki ijayo kuanzia tarehe 4-6 Mei. Semina itaendeshwa na Mch. Douglas Mmari kutoka Minnesota. Kutakuwa na waimbaji maarufu wakiongozwa na Dada Flora Mbasha kutoka Tanzania na Printze Ngosso wa hapa Columbus. Kwa maelezo zaidi ingia kwenye hii link.

Sherehe za Muungano zafana Nchini Uingereza

Urban Pulse na Miss Jestina Blog wanakuleta taswira ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika hapa Tottenham, london Jumamosi tarehe 28.4.12.

Sherehe hii ilihudhuriwa na wadau mbalimbali, Mgeni rasmi alikuwa balozi wetu Mh Peter Allan Kallaghe akifuatana na mkewe, Naibu balozi pamoja na baadhi ya maofisa wa Ubalozi wetu hapa jijini London.

Aidha wakati akitoa hotuba yake Mh Balozi Kallaghe ailiwashukuru wadau na watanzanzia wote waliojitokeza leo kuja kuadhimisha sherehe hii na kuwasihi kuendeleza kudumisha muungano wetu uliodumu kwa miaka 48 sasa. Pia aliwaomba wadau wote kuendelea kufuatilia mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya ya nchi yetu unaondelea nyumbani.

Kwa picha zaidi za matukio bofya hapo chini
http://www.jestina-george.com/2012/04/taswira-za-sherehe-za-muungano-wa.html#more

Sherehe hii iliandakiwa na Swift Freights UK pamoja na Pit Stop ” Uwanja wa Nyumbani”

Asanteni,


Mh.balozi wa Tanzania Uingereza Peter Allan Kalaghe akitoa hotuba juu ya muungano.
Mh.balozi Kallaghe na mkewe wakifungua muziki.
Mh.Naibu balozi Kilumanga akicheza na Mchumba wake Irene.

wadau wakiruka majoka.
Wakati wa cheers.