Afrika Kusini na Kenya wako juu kwa matumizi ya Twitter Afrika.

Uchunguzi mpya unasema raia wa Afrika kusini na Kenya kuwa ni watumiaji wakubwa wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kwamba hivi sasa mtandao huo wa kijamii unakua haraka na kuwa nyenzo kubwa ya mawasiliano kwenye bara hilo.

Kwa mujibu wa VOA wachunguzi wametafiti zaidi ya twitt milioni 11.5 kutoka maeneo fulani ya Afrika katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2011.

Wamegundua Afrika kusini imetuma zaidi ya twitt milioni 5 , ikiwa ni mara mbili zaidi ya watu katika nchi nyingine. Kenya ilikuwa ya pili ikiwa na karibu milioni 2.5 , ikifuatiwa na Nigeria, Misri na Morocco.

Katika uchunguzi huo iligundulika asilimia 80 ya wale walioulizwa walitumia twitter kuwasiliana na marafiki zao, karibu asilimia 70 walitumia kupata habari na watu juu kidogo ya asilimia 20 walitumia mtandao huo kutafutia kazi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 27 other followers