Kiongozi wa Alqaeda wa Ymen aliyekuwa akijificha katika milima ya nchi hiyo Anwar Al Awlaki ameuwawa na mashambulizi ya bomu ya vikosi vya Marekani.
Amekuwa ni Mmarekani wa kwanza kuuwawa kwa amri ya Whitehouse katika shambulizi kila mabomu lijulikanalo kama Operesheni Troy. Al Awlaki ni mzaliwa wa Marekani na amewahi kuwa Imam wa msikiti mmoja wa Alexandria Virginia.
Kwa mujibu wa jarida la Usa today Al awlaki alishiriki katika kupanaga mashambulizi kadhaa dhidi ya Marekani ikiwa ni pamoja na bomu lililoshindwa kulipuka lililofichwa kwenye nguo ya ndani na raia wa Nigeria Abdul Mutalab. Pia amehusishwa na Meja Haassan Nidal aliyefyatua risasi na kuuwa wanajeshi kwnye kambi ya jeshi huko Texas.
Serikali ya Obama kwa mara nyingine imeonyesha uwezo wake wa kupambana na ugaidi nje ya Marekani kwa staili ya kuwaondoa wakuu wa mitandao lakini safari hii kuna utata kutoka kwa wakosoagi wa serikali wakidai kwamba raia wa Marekani hawezi kuuwawa kwa staili hiyo bila kupata kwenda mahakamani.
Lakini serikali ya Obama imeshaeleza kuwa mtu huyo alikuwa kwenye orodha ya CIA ya maadui wanaotafutwa au kuuuwawa kwa sababu ni adui wa nchi. Baba yake Al awlaki kwa upande wake aliwahi kupinga uamuzi huo wa serikali mahakamani lakini alishindwa.












