Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesheherekea sikukuu ya uhuru ikiwa hivi sasa ni miaka 51 tangu nchi hiyo ijikwamue kutoka ukoloni.
Japokuwa wananchi wametoka katika ukoloni huo lakini hali ya wananchi wakawaida haijaboreka bado.
Sherehe za Alhamisi zilifanyika mjini Lubumbashi jimboni Katanga zikihudhuriwa na Rais Joseph Kabila.
Na huko mashariki mwa nchi hiyo hasa mjini Goma kulikuwa na gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha sherehe hizo.





