NATO kuendeleza majamboz Libya

Kamanda wa NATO wa operesheni ya Libya anasema majeshi ya muungano hayapunguzi mashambulizi ya anga licha ya wito wa baadhi ya mataifa kusimamisha operesheni hiyo.

Luteni Jenerali wa Canada Charles Bouchard amesema operesheni hiyo inayoingia mwezi wa nne imepata maendeleo makubwa na kwamba mashambulizi dhidi ya raia na serikali ya Libya yamepungua.

Kwa mujibu wa VOA maelezo ya NATO yamekuja wakati mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu akiwataka wasaidizi wa Moammar Gadhafi wamkamate na wamfikishe kwenye mahakama hiyo kujibu kesi.

Soma zaidi bofya Maelezo hayo ya Luis Moreno Ocampo hii leo yamekuja baada ya mahakama iliyoko The Hague kutoa hati jana ya kukamatwa kwa Bw.Gadhafi na wasaidizi wake wakuu wawili kwa makosa ya uhalifu wa kivita yanayohusiana na kukandamizwa kwa uasi wa upinzani.

About these ads

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,705 other followers