Archive for June 16, 2011

Posted in Uncategorized on June 16, 2011 by sunday Shomari

Makundi mawili ya utetezi wa kisheria huko afrika kusini yanabisha uamuzi wa rais Jacob Zuma kuongeza muda wa muhula wa jaji mkuu. Makundi hayo yamesema Bwana Zuma huenda amekiuka madaraka yake ya kikatiba kwa kuchukua uamuzi huo mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa VOA wamesema watafikisha mashtaka yao mbele ya mahakama kuu ya Pretoria. Rais Zuma alitangaza Juni tatu kwamba alikuwa anaongeza muda wa muhula wa jaji mkuu Sandile Ngcobo kwa miaka mitano mingine mpaka augusti 2016. Jaji huyo alitakiwa kujiuzulu miezi miwili kutoka sasa baada ya kutumikia kwa miaka 12 inayokubalika katika katiba ya mahakama.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,707 other followers