Archive for June 6, 2011

Posted in Uncategorized on June 6, 2011 by sunday Shomari


Mh. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe akifungua mkutano wa Diaspora II huko London.(Picha kwa hisani ya Michuzi)

Mbowe Mbaroni.

Posted in Uncategorized on June 6, 2011 by sunday Shomari


Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam kufuatia agizo la pili la Hakimu wa Mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali mkoani Arusha tarehe 5 Januari 2011.

Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria katika mahakamani hapo Mei 27, 2011, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na Polisi.

Mahakama hiyo awali iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini), Bi. Josephine Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.

Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani, hata Mawakili wao, Bw. Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini washtakiwa Bw. Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Bw. Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwa wakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.

Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Nai Steven, Mathias Valerian, John Materu, Daniel Titus, Juma Samuel, Walter Mushi, Peter Marua na Erick Makona.

Hakimu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo wala mdhamini wake, hivyo Ofisa mhusika wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo, “wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa mhusika amkamate na kufikishwa mahakamani.”

CHANZO:http://www.wavuti.com/

Miss Lindi 2011.

Posted in Uncategorized on June 6, 2011 by sunday Shomari


Mrembo Loveness Flaviana jana usiku alivishwa taji la Miss Lindi 2011 katika ukumbi wa Lindi Oceanic. Taji lililokuwa likishikiliwa na Mary Adam Miss Lindi (2010).
PICHA KWA HISANI YA MDAU ABDULAZIZ)

Watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa m/kiti wa CCM wilaya ya Rungwe wafikishwa mahakamani

Posted in Uncategorized on June 6, 2011 by sunday Shomari

Na Francis Godwin wa Francisgodwin.blogspot.com kutoka Mbeya
Bw.Joachim Nyambo anaripoti kuwa Watu nane leo wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wakikabiliwa na shitaka la mauaji ya aliye kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani humo.

Washitakiwa hao nane kati ya 11 wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kuhusika na tukio hilo wamefikishwa mahakamani majira ya saa 10 jioni.

Washitakiwa hao ni Akimu Mwakalinga(40) mkazi wa Ilundo wilayani Rungwe,Fredy Nkwaba(57) mkazi wa Kiwira,Jumanne Mwakisole (46) mkazi wa Kiwira,Yusuf Asukile (29) mkazi wa Uyole jijini Mbeya,Furaha Wanyangi(36) mkazi wa Makandanda Rungwe,Joshua Mwasakene maarufu kama Lyope(42) mkazi wa Kiwira,Abrahamu Mwanyombole(51) mkazi wa Mpandapanda na Adeso Mwakipesile (41).

Imeelezwa na Mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa Polisi Samuel Saro mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Omary Kingwele kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo mei 19 mwaka huu nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Mpandapanda kilichopo katika kata ya Kiwira.

Mwendesha mashitaka huyo amesema washitakiwa hao walitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 196 cha sheria cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2002 baada ya kufanyiwa marekebisho

Hata hivyo kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza mashitaka ya mauaji,washitakiwa wote nane hawakutakiwa kujibu lolote juu ya shitaka linalowakabili na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 17 mwaka huu itakapotajwa.
Francisgodwin.blogspot.com

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,706 other followers