Timu ya taifa ya Mexico.
Timu ya taifa ya Mexico jumamosi ilithibitisha kutangulia si kufika baada ya kutoka nyuma wakiwa wamepigwa bao 2-0 na hatimaye kurudisha yote na kushinda kwa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya timu ya taifa ya Marekani.
Mechi hiyo ikiangaliwana watazamaji zaidi ya 90,0000 ilianza taratibu huku kila mmoja akimsoma mwenzake na ndipo Marekani walipopata bao 2 za haraka haraka.
Baada ya Landon Donovan kupachika la pili Mexico walikuja juu na kusawazisha mabao hayo ambayo yalidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mexico kucheza kwa kasi na kupachika bao la tatu na hatimaye walipachika msumari wa mwisho kwenye jeneza la Marekani kwa kufunga goli la nne baada ya kipa mkongwe Tim Howard kutoka golini kujaribu kuokoa hatari golini mwake kutoka kwa mshambuiaji hatari wa Mexico Giovanni Dos Santosh aliyepachika bao la nne.
Mpaka mwisho wa mchezo Mexico 4 na Marekani 2. Hivyo Mexico ndio mabingwa wa CONCACAF 2011 naye Javier Hernandez alikuwa mfungaji bora wa michuano kwa kupachika mabao 7. Wakati mchezji bora wa mechi hiyo alikuwa Giovanni Dos Santosh.