
Dj Kevin Twissa na kiongozi na mjasiria mali kutoka Daressalaam Tanzania akifanya vitu vyake Columbus Ohio.
Archive for May, 2011
Picture of the Day
Posted in Uncategorized on May 31, 2011 by sunday ShomariMambo ya Memorial weekend Ohio
Posted in Uncategorized on May 29, 2011 by sunday Shomari
D j Luke (kushoto), Pam lolo na Abraham katika usiku wa Ijumaa uliokuwa na vionjo vya Afrika mambo moto Ohio a.k.a Buckeye state. (Picha kwa hisani ya Dj Luke Joe).

Hapo chini Jackie Twissa a.k.a Sr. J (kushoto) akiwa na Mama Enid Fisher katika mambo ya Ijumaa. Kwa picha zaidi Bofya Read more »
Siku Chitu alipobadilisha status
Posted in Uncategorized on May 29, 2011 by sunday Shomari
Mtalaam na aliyekuwa Sr. Bachelor Bw. Chitumbi a.k.a Chitu siku alipoaga rasmi ukapela jijini Daresalaam Tanzania akiwa na mkewe mpenzi hongera Chitu na kwaheri kwenye kilabu cha Ma Sr. Bachelor umefukuzwa rasmihivi sasa.
Baskeli ya mbao
Posted in Uncategorized on May 26, 2011 by sunday Shomari

Huu ni utaalam wa baskeli iliyotengenezwa kwa mbao ulionaswa na mwandishi wa Sauti ya Amerika Goma Reuben Lukumbuka.
Mnyarwanda kizimbani Marekani kwa mauaji ya halaiki ya Rwanda 1994 .
Posted in Uncategorized on May 26, 2011 by sunday Shomari
Jopo la wataalamu wa sheria katika jimbo la Kansas hapa Marekani limeanza kusikiliza kesi ya mhamiaji mmoja mtu mzima anayeshutumiwa kwa kushiriki katika mauaji ya halaiki miaka 17 iliyopita nchini Rwanda.
Kwa mujibu wa VOA waendesha mashitaka na mawakili wa utetezi walimaliza kutoa maelezo yao jumatano kwenye kesi dhidi ya Lazare Kobagaya.
Mtu huyo mwenye umri wa maika 84 anashitakiwa kwa kudanganya maafisa wa uhamiaji kuhusu historia yake ili kupata uraia wa Marekani 2006.
Maafisa wa uhamiaji wanasema alijaza kwenye fomu za uhamiaji kwamba aliishi Burundi wakati wa mauaji ya halaiki ya 1994 nchini Rwanda na kukana kabisa kufanya uhalifu wowote.
Uingereza na Ufaransa washusha helikopta Libya
Posted in Uncategorized on May 24, 2011 by sunday Shomari
Uingereza na Ufaransa wameamua kupeleka helikopta zakushambulia ili kujiunga na kampeni za NATO dhidi ya majeshi ya kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi.
Kwa mujibu wa VOA waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Alain Juppe amesema leo Jumatatu kuwa upelekaji uko katika misingi ya mamlaka ya ya Umoja wa Mataifa kuwalinda raia wa Libya. Amesema hilo litafanyika haraka iwezekanavyo.
NATO ina takriban ndege za kivita 200 kwa ajili ya operesheni zake nchini Libya, lakini haijatumia helikopta zozote kufanya mashambulizi ya kuyapiga majeshi ya Gadhafi ambayo yanawatishia raia.
Obama apongeza juhudi za amani Ireland
Posted in Uncategorized on May 23, 2011 by sunday Shomari
Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara huko Ireland kwa kupongeza juhudi zao za kuleta amani katika jimbo la Uingereza la Ireland kaskazini na kusema inatia moyo Marekani.
Kwa mujibu wa VOA baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ireland Enda Kenny huko Dublin leo Bw. Obama amesema “maendeleo kuelekea amani Ireland kaskazini yanaonyesha kwa jinsi gani watu wanavyoweza kuangalia upya mahusiano yao katika mapambano ya muda mrefu”.
Rais pia alisema ziara ya kihistoria ya Malkia Elizaberth huko Ireland wiki iliyopita imewasaidia kuleta uhusiano mzuri baina ya pande zote mbili na inaleta “wimbi la matumaini” kwa mataifa mengine duniani. Ziara ya Malikia Elizabeth ilikuwa ya kwanza kwa ufalme huo huko Ireland katika muda wa karne nzima.
Sudan kaskazini yaendelea kudhibiti Abyei.
Posted in Uncategorized on May 23, 2011 by sunday Shomari
Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan umeripoti kutokea uchomaji moto na wizi katika mji wa Abyei unaogombaniwa ambao Sudan kaskazini ulichukua udhibiti wake siku mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa VOA katika taarifa yake ujumbe huo umelaani vikali ghasia zinazoendelea jumatatu na umesema jeshi la kaskazini linawajibika kushikilia sheria katika eneo linalodhibiti.
Umoja wa mataifa inalaumu uchomaji moto na wizi unaofanywa kwa kutumia silaha. Lakini taarifa ya UN haikufafanua zaidi.
Mapema jumatatu wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa walitaka Sudan kaskazini kuondoa majeshi yake huko Abyei .
Picture of the Day
Posted in Uncategorized on May 22, 2011 by sunday Shomari
Kutoka kushoto Mama Mhando,wahitimu Elinita na Dr.Haika Mhando pamoja Mama Mchungaji Kashaa na Mchungaji Kashaa katika sherehe maalum ya kuwapongeza wahitimu hao huko Atlanta Georgia. Kwa picha zaidi bofya Read more »
Bernard Hopkins avunja rekodi ya Foreman
Posted in Uncategorized on May 22, 2011 by sunday Shomari
Bernard Hopkins alidhihirisha jumamosi kuwa uzee ni dawa kwa kuvunja rekodi ya George Foreman ya kuwa bingwa dunia wa uzito wa Light Heavy baada ya kumtwanga Jean Pascal wa Canada kwa pointi nyingi mbele ya mashabiki 17,750 kwenye ukumbi wa Bell Arena Canada.
Bernard Hopkis ambaye alilalamika kuwa alinyimwa ushindi katika mchezo wao wa kwanza na kuthibitisha kuwa yeye bado ni moto wa kuotea mbali. Hopkins sasa ameweka rekodi ya kuwa bingwa mwenye umri mkubwa kliko wote akiwa na umri wa miaka 46.
Jean Pascal ambaye ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 28 alitamba kuwa Hopkins ni mzee mno na akijaribu kurudiana nae atakiona chamoto lakini mambo hayakuwa kama alivyosema na alijikuta akilambishwa mchanga ni kushambuliwa katika raundi karibu zote.
Bernard Hopkins alisema wazi kupitia HBO kuwa Pascala liridhika na matokeo ya awali ya “Droo” kwasababu alijua alibebwa na alimweleza wazi kuwa Pascal ni bondia wa raundi 4.



